KERO Viwanda vinafanya Kibaha eneo la Zogowale kuwa sio mahali salama kuishi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Keyboard_Warrior

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
6,381
Reaction score
11,296
Mimi ni mkazi wa Kibaha-Zogowale, eneo ninaloishi limezungukwa na viwanda. Hivi karibuni kumeibuka shida kubwa ya uchafuzi wa hali ya hewa wakati wa usiku. Kuna harufu kali sana inachafua hewa wakati wa usiku, nina uhakika harufu hii si salama kwa afya ya binadamu.

Viwanda ni chachu ya maendelo ya taifa, ila serikali inatakiwa kuangalia ni namna gani maendeleo ya viwanda hayaleti madhara makubwa ya afya kwa raia wake.

NEMC na taasisi zingine za serikali zenye mamlaka ya kufuatilia kero hii njoeni Kibaha muangalie namna ya kutatua changamoto hii, KWANI KIBAHA PAMEKUWA SI MAHALI SALAMA KUISHI.
 
Changamoto za maendeleo na uwek3zaji wa viwanda.......safari bado ndefu sanaaaa
 
Viongozi wa serikali ya mtaa hata sijui wanafanya kazi gani!?

Tunateseka sana mkongwe, hiyo harufu ikianza usingizi unakata ghafla.
Mtaa mzima unanuka, harufu inaenda hadi kwenye koo inakereketa.
 
Njaaaa sanaaa .....serikali mtaa njaa sanaa sio kosa lao.....
 
Viongozi wa serikali ya mtaa hata sijui wanafanya kazi gani!?

Tunateseka sana mkongwe, hiyo harufu ikianza usingizi unakata ghafla.
Mtaa mzima unanuka, harufu inaenda hadi kwenye koo inakereketa.
Nyie ndio mlikifuata kiwanda au kiwanda kilikuja kikawakuta??
 
Ishi angalau 2km kutoka kiwanda kilipo.
Kwa nini serikali haiweki mipango miji kutenganisha maeneo ya viwanda vya uchakataji bidhaa ngumu na kemali mbali na makazi ya watu?
 
Lishaitwa eneo la viwanda.. ni bora kutafuta ustaarabu mwingine wakati unasubiri kuhamishwa ili kunusuru afya yako
 
Sisi huku wakaz wa kimbiji kigamboni tumevamiwa.na malaya yaan hapa lake cement company ikifika.jion n kama tupo uwanja wa fisi kwel maendeleo huja na karaha
Vipi mwajuma wako ndala ndefu naye..

Nyau wewe
 
Mimi ni mkazi wa Kibaha-Zogowale, eneo ninaloishi limezungukwa na viwanda. Hivi karibuni kumeibuka shida kubwa ya uchafuzi wa hali ya hewa wakati wa usiku. Kuna harufu kali sana inachafua hewa wakati wa usiku, nina uhakika harufu hii si salama kwa afya ya binadamu.

Viwanda ni chachu ya maendelo ya taifa, ila serikali inatakiwa kuangalia ni namna gani maendeleo ya viwanda hayaleti madhara makubwa ya afya kwa raia wake.

NEMC na taasisi zingine za serikali zenye mamlaka ya kufuatilia kero hii njoeni Kibaha muangalie namna ya kutatua changamoto hii, KWANI KIBAHA PAMEKUWA SI MAHALI SALAMA KUISHI.
NEMC ni wala rushwa wabobevu usitegemee watasaidia.
 
NEMC hiki kiwanda cha karatasi/maboksi Zogowale Kibaha kitatuua, hii harufu inatunyima usingizi.
 
Back
Top Bottom