Sikirimimimasikini
JF-Expert Member
- Dec 27, 2019
- 2,926
- 15,634
Cc: let the caged bird sings,
Uturiki yaripoti kuwa viwanda mbalimbali nchini Netherlands vinafungwa kwa 'fujo' (wingi) kutokana na bei ya nishati kuongezeka zaidi. Hiyo ni kutokana na Urusi kuamua kuzinyoosha nchi za EU kwa kuwanyima gesi yake. Gharama za uzalishaji zimekuwa kubwa zaidi kiasi kwamba wamiliki wa viwanda wameona ni upuuzi viwanda vyao kuendelea kuzalisha bidhaa kwa hasara.
Viwanda vilivyoathirika zaidi ni vile vya kuchakata metali kama vile viwanda vya kuzalisha chuma, chuma cha pua (steel), aluminium, shaba na zinki. Pia sampuli nyingine za viwanda vinavyofungwa ni viwanda vya kutengeneza aina mbalimbali za karatasi ikiwemo zile tunazoziita Bongo RIM paper, viwanda vya vyakula na viwanda vya kemikali mbalimbali ikiwemo mbolea.
=====