Jamani, hivi sukari imeanza kupungua mwaka huu?? Miaka yoote, mbona hatujafikia hapa? Kuna sababu. Ushauri wangu ni kwamba, serekali iwatafute watu competitive wenye nia ya dhati kabisa kuzalisha sukari, wawape mkono ili wapewe mkopo na TIB, waanzishe kilimo cha miwa na wakifikia uzalishaji, wapewe vinu vya kusindikia wazalishe sukari. Yaweza chukua mda lakini watazalisha ule upungufu uliopo kutokana na viwanda vyetu kutokidhi hitaji hilo.
Ardhi tunayo, uwezo tunao ila nia hatuna na hilo latokana na wakuu wenyewe kuwa, yawezekana watu wakafaidi. Ule uwezo wa kutengeneza juice tu, uongezwe tuweze kutengeneza sukari na tooth pick pia.