Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 170
- 445
Viwanda vya kusafisha mafuta ( oil refineries) vya barani Ulaya vimeanza kuonja joto la jiwe baada ya kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote kuanza kufanya kazi.
Kiwanda hicho cha Dangote ambacho ni miongoni mwa viwanda vikubwa zaidi vya kusafisha mafuta duniani kimesababisha viwanda vya mafuta vya Ulaya vilivyokuwa vikitegemea soko la Afrika hasa Afrika magharibi kukosa soko kutokana na ushindani ulioletwa na kiwanda cha Dangote .
Viwanda hivyo ambavyo vingi vilikuwa vinazalisha mafuta yaliyo chini ya viwango vinavyokubalika barani Ulaya vimekumbwa na hali mbaya na hata baadhi yake kufungwa baada ya bidhaa zao kukosa soko.
Mfano, mnamo tarehe 25 Novemba 2024, kiwanda cha kusafisha mafuta cha Gunvor Rotterdam Refinery cha nchini Uholanzi kilifungwa kwa sababu ya kujiendesha kwa hasara.
Soma Pia: Dangote aeleza alivyonyimwa Mafuta na Nchi yake Nigeria. Hata alipotaka kuagiza ya nje alinyimwa kibali
Pia, waendeshaji wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Grangemouth cha Scotland ambao ni PetroIneos wameeleza kuwa watakifunga kiwanda hicho ifikapo mwakani 2025 . Sababu iliyotajwa na waendeshaji hao ni ushindani mkali ulioletwa na viwanda vingine vya usafishaji mafuta.
Uanzishwaji wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote ulitarajiwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye biashara ya mafuta kati ya Ulaya na Afrika hasa Afrika magharibi.
Vyanzo/Sources:
Business NG
Vanguard
Thisdaylive
Reuters
"Nigeria's Dangote oil refinery could accelerate European sector's decline | Reuters" https://www.reuters.com/business/en...celerate-european-sectors-decline-2024-03-27/