Viwango hivi vipya vya nauli ni vikubwa mno

Viwango hivi vipya vya nauli ni vikubwa mno

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KATUNI(761).jpg

Maoni ya katuni.


Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imetangaza viwango vipya vya nauli za mabasi, treni na gharama za bandari zitakazoanza kutumika Aprili 12, mwaka huu.

Viwango hivyo vya nauli vinahusu usafiri wa reli ya kati, mabasi yaendayo mikoani na daladala katika Jiji la Dar es Salaam. Pia gharama mbalimbali za bandari zikiwamo tozo za nahodha kuingiza meli katika bandari zilizoko chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) zimepanda kwa asilimia 34.3.

Sumatra inasema viwango hivyo vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za sheria na za kiutendaji kama wamiliki wa vyombo vya usafiri walivyoomba.

Kwa mujibu wa Sumatra, wamiliki wote wa mabasi, Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na TPA na kuwa kila mmoja ilipeleka mapendekezo ya kuomba viwango vya nauli kuongezeka na kuwa baada kupokea maombi hayo yaliyotoka kwa kila upande iliamua kukaa na wadau na wamiliki vyombo vya usafiri ili kusikiliza maoni yao kabla mamlaka hiyo kufanya maamuzi ya mwisho.

Wamiliki wa daladala walipendekeza kupandishwa kwa nauli kwa asilimia 149 wakati wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani walipendekeza asilimia 35 hadi 48.5 kutokana na ongezeko la gharama za uendeshaji.

Hata hivyo, Sumatra iliamua kuongeza viwango vya juu vya nauli za daladala kwa wastani wa asilimia 24.46 na kuongeza viwango vya mabasi yaendayo mikoani kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida na asilimia 16.9 kwa mabasi ya daraja la tatu na asilimia 13.2 kwa mabasi ya daraja la juu.

Kwa upande wa daladala nauli ya wanafunzi imepanda kutoka Sh. 150 hadi Sh. 200 wakati nauli ya mtu mzima imepanda kutoka Sh. 300 hadi Sh. 400-700 kulingana na umbali katika Jiji la Dar es Salaam.

Kuhusu nauli za treni ya kati, TRL iliwasilisha maombi kwa Sumatra kupitia upya viwango vya nauli na kuomba ongezeko la asilimia 50 ya nauli kwa abiria wa daraja la tatu na ongezeko la asilimia 25 kwa daraja la kwanza na la pili.

Hata hivyo, baada ya mamlaka kufanya tathmini kwa kuzingatia vigezo kadhaa kama gharama za utoaji huduma, iliridhia viwango vipya vya nauli kwa madaraja yote na kuamua kuongeza nauli za daraja la kwanza na la pili kwa asilimia 25 na asilimia 44 kwa daraja la tatu.

Kimsingi, viwango vilivyotangazwa ni vikubwa mno kulingana na hali ngumu ya maisha kwa wananchi wengi hususani wenye kipato cha chini. Kwa maana hiyo, hatua hiyo itaongeza ukali wa maisha ya wananchi ambao wamekuwa wakilalamikia hali ngumu ya maisha kila uchao.

Ni kweli kwamba watoa huduma za usafirishaji wanakabiliwa na gharama kubwa za uendeshaji, lakini lingekuwa jambo la busara kwa Sumatra kutangaza ongezeko la nauli baada ya kusubiri kusomwa kwa bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2013/14 katikati ya Juni, mwaka huu.

Ni katika mkutano wa Bunge wananchi hususani wafanyakazi wanatarajia kwamba serikali itatangaza kima kipya cha chini cha mshahara ambacho wamekuwa wakikidai kwa muda mrefu kiongezwe kutoka Sh. 200,000 hadi Sh. 315,000.

Kwa kusubiri kutangazwa kwa kima cha chini cha mshahara kabla ya kupandishwa kwa nauli angalau Sumatra ingeonekana kujali pande zote mbili yaani wasafirishaji na watumiaji wa huduma za usafiri.

Hata hivyo, kitendo cha Sumatra kutokuwa na subira kinaweza kuchukuliwa kwamba mamlaka hiyo imeangalia upande mmoja. Kwa maana nyingine, imewapendelea wafanyabiashara na kuwaacha maskini wakihangaika.

Kwa muda mrefu tumekuwa tukiwashuhudia wafanyabiashara wa usafirishaji wakishinikiza kupandishwa kwa nauli hata kama hakuna sababu za msingi huku wakitumia kizingizio cha kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Kwa bahati nzuri Sumatra mara nyingi imekuwa ikiwakatalia na kuamua kuitisha mikutano ya wadau kujadili na baadaye kufanya utafiti na kutangaza kukataa maombi ya wasafirishaji.

Ndiyo maana wamiliki wa daladala waliwasilisha Sumatra maombi ya kupandisha nauli kwa asilimia 149 na mamlaka kushusha hadi asilimia 24.46.

Kwa kuwa siku zote nia ya mfanyabiashara ni kupata faida kubwa, madai vya watoa huduma za usafirishaji kwamba gharama za uendeshaji zimepanda hayana msingi kwa kuwa kama wangekuwa hawapati faida wangeachana na biashara hiyo na kufanya shughuli nyingine.

Kibaya zaidi ni kwamba wafanyabiashara hao wanaoshinikiza kupandishwa kwa nauli hawazingatii sheria, kanuni na taratibu. Kwa mfano, wamiliki wa mabasi ya mikoani kila unapofika mwisho wa mwaka, hupandisha nauli kwa kiwango cha juu bila baraka za Sumatra.

Kwa daladala za Dar es Salaam siku zote zimekuwa zikikatisha ruti, kupandisha nauli, lugha chafu za madereva na makondakta na kero nyingine. Kwa bahati mbaya sana haya Sumatra imeshindwa kuyadhibiti na ndiyo maana hatua ya kupandisha nauli imepokelewa kwa mtazamo hasi.

Kwa msingi huo, sisi tunashauri kwamba suala hili la kupanda kwa viwango vya nauli, liangaliwe upya ili kuwe na uwiano mzuri kati ya pande mbili yaani wafanyabiashara na watumiaji wa huduma hiyo ya usafiri.

Iwapo hali hii itaachwa kama ilivyo sasa, ni sawa na kupendelea upande mmoja wa mfanyabiashara huku upande wa pili yaani mwananchi anayetumia huduma ya usafiri ukipata maumivu makali.






CHANZO: NIPASHE

 
Punda afe mzigo ufike. Tunatekeleza sera za ccm.
Upande mwingine ukiangalia kwa mfanyabiashara spare za magari zimepanda bei sana na bado bei ya mafuta ni tete. Nchi haina mwenyewe hii.
 
Punda afe mzigo ufike. Tunatekeleza sera za ccm.
Upande mwingine ukiangalia kwa mfanyabiashara spare za magari zimepanda bei sana na bado bei ya mafuta ni tete. Nchi haina mwenyewe hii.
King'asti sijui kwanini CCM wamekuwa hivi walivyo na sera yao ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA sion kama imekusudiwa kufikisha lengo kabisa. imainie sasa hivi usafiri wa daladala hapa DSM kila siku asbh na jion kwa wasiokuwa na magari yao binafsi basi wanapanda viDAR GUMZO (zile canter ndogo kabisa) tena kwa nauli ya sh 1000-2000 kwa ruti.


abiria sio wa mbezi wala wa gongo la mboto ama wa tabata wanaopata raha ya usafiri sasa sijui kama wanaongeza nauli ilihali hakika wa usafiri haupo wana maanisha nini. imagine mtu ambaye serikali ina uhakika wa kupata kodi yake kila mwezi lakin bado haimsadii hata kumwekea wezo wa kusafiri kwa uhakika kila atokapo kazini ama aendapo. Fikiria watu kupanda dar gumzo kama basi inatia hasira kuliko hata zile chai maharage za miaka ya 90. na hapa imeonyesha sisi kurudi nyuma kwa hatua mia zaid kulikomiaka ya 90.

sasa je MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA NI HAYA??? JE KWELI HATA USAFIRI WA DALADALA SERIKALI INASHINDWA KUTUWEKEA UTARATIBU MZURI JAPO SISI TUNAULIPIA??


nimeskia na hapa naomba watu wasukunuku wanidadisie vyema eti kwasasa serikali hairenew TLB za daladala once ikisha expire simply ni kwasababu eti ya mabasi yaendayo kwa kasi jiulize hata njia tu ya kupita bado haijakamiliaka na haijulikan itakamilika lini sasa kwanini waondoshe hizi daladala mapema??

kupandisha nauli bado ni kutuumiza tu manake hata hizi nauli hazituthibitishii kupata uhakika wa usafiri.
 
Last edited by a moderator:
Iwapo hali hii itaachwa kama ilivyo sasa, ni sawa na kupendelea upande mmoja wa mfanyabiashara huku upande wa pili yaani mwananchi anayetumia huduma ya usafiri ukipata maumivu makali.

kuna hiki chombo kinaitwa Sumatra na kingine kinaitwa Ewura na kazi zao zinashahibiana maana bila kiwese usafiri hakuna. Ewura anaongeza bei ya mafuta lakini hatafakari nauli na huyu anatafakari nauli lakini siyo bei ya mafuta. Ushauri wangu vyombo tajwa viunganishwe ili tujue wa kumkaba koo ni yupi mbali ya kupunguza gharama za uendeshaji wa vyombo vyenyewe. Jingine hawa Ewura walianzisha mpango wa "bulky" ambao matunda yake ni kuwa ulaji wanaukusanya kwa urahisi lakini wameua ushindani wa soko na hivyo kutufanya tuwe teja ya wafanyabiashara waovu ambao hupanga bei waitakayo na kama hatutaki wanatutishia kutoleta mafuta....................huu ufisadi wa Ewura ndiyo chimbuko la shida zote.
 
Back
Top Bottom