viwango vipya vya ufaulu kwa kidato cha sita kuongezwa ni busara wakati huu?

Joined
Apr 5, 2013
Posts
18
Reaction score
3
Ndugu wana JF wakati huu ambapo jamii ya watanzania wameduaa wasijue cha kufanya baada ya mshtuko wa kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana ambapo hata jawabu la tatizo hilo bado linatafutwa na serikali kwa kuunda hata tume za uchunguzi,Baraza la mitihani (NECTA) limeongeza viwango vipya vya ufaulu kwa wanafunzi walio kidato cha sita sasa hivi.Swali ninalo jiuliza ambalo katika hali ya kawaida lilitakiwa kujibiwa na mwendeshaji wa mitaala (curricular developer) je kumekuwa na ufaulu mkubwa sana kwa wanafunzi hawa kiasi cha kufikiria kuwa wanafunzi wanapata alama za ufaulu kwa urahisi bila bidii inayotakiwa? au ni kutuandalia sisi wananchi kilio kingine mwaka kesho? je kwa nini swala la Elimu linakuwa rahisi kuibuliwa na kutekelezwa kiasi hiki? je watendaji wanajua haya ni maamuzi nyeti yanayohusu maisha ya watanzania wengi?.Mfano wa swala hili kuliona wanalifanyia mzaha ni pia katika kudahili wanafunzi ambako walioko kidato cha sita sasa hivi awali walielewa kuwa watafanya mitihani yao mwaka kesho mwezi wapili kama ilivyokuwa kawaida.Ghafla wamebadilishiwa utaratibu na sasa mitihani hiyo wataifanya mwezi wa tano mwaka kesho.Je kwanini hili halikufahamika tangu mwanzo?
 

Attachments

  • A Level grading.jpg
    107.7 KB · Views: 862
Tuwekee hvyo viwango alafu elimu ambayo ni kwa ajiri ya ukombozi wa fikra kwanini wananchi hawapewi fursa kujadili kwanz
 
inamaana hivyo viwango vipya vya Ufaulu vimewahusisha hata wale wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mapema mwaka huu au vitaanza kutumika rasmi kwa wale watakaomaliza kuanzia mwakani.?
 
Viwango hivyo vitaanza kutumika mwakani.Swala ni kuwa kama mwanafunzi kuanzia mwaka jana alipo anza kidato cha tano kwa mfano alikuwa akipata 50 alihesabiwa daraja C.mwaka kesho katika maendeleo ya mwanafunzi huyo huyo wakitaka historia ya maendeleo yake sasa mfumo mpya atakuwa daraja E.Je ni sawa? je kulikuwa na udharula wowote wa kufanya hayo?
 

Duh! hawa jamaa wanampango wa kutumaliza!
 
waseme basi lengo hapa ni nini? kupunguza wanaojiunga univ. ama mtihani imekuwa myepesi mno siku hizi
 
Mkuu usishangae kwani hiyo ndiyo elimu yetu, Mfano kumbe tokea 2010 NECTA walibadili alama za ufahulu C ikawa inaanzia 50-65 badala ya 41, na D ikawa inaanzia 35-49 na sio 21-41 kama ilivyozoeleka alafu leo hii wanaanza kutapatapa mara kuunda tume..
 
Sioni sababu ya watanzania kulalamika katika hili.

Suala la msingi ni kwamba viwango vyetu vya alama ni lazima viwe na uwiano sawia na vya kimataifa.

Yeyote humu JF anaeilaumu NECTA atakuwa ni mvivu wa kufanya tafiti tu, kwa muda mrefu sasa NECTA wamekuwa wakitumia viwango vya chini vya alama kulinganisha na vile vya kimataifa.

Jambo la msingi hapa ni; tusiilaumu NECTA, ilaumiwe WIZARA yenye dhamana husika, yenye jukumu la kuitekeleza sera ya elimu.
 
Mkuu usishangae kwani hiyo ndiyo elimu yetu, Mfano kumbe tokea 2010 NECTA walibadili alama za ufahulu C ikawa inaanzia 50-65 badala ya 41, na D ikawa inaanzia 35-49 na sio 21-41 kama ilivyozoeleka alafu leo hii wanaanza kutapatapa mara kuunda tume..

Hii habari imepingwa vikali sana, tena sana na NECTA. Hata kwenye toleo la Raia Mwema (la kwenye mtandao) kuna hiyo habari; habari hiyo inahusiana na kufeli kwa Kidato cha Nne, 2012.
 

Ili kweka habari sawa, JE HIVI NI VIWANGO VYA KIMATAIFA? Kama 'NDIYO', ahsante sana NECTA kwa kuwa Watanzania tunapaswa kwenda sawa na upepo.

Ila hofu yangu, pamoja na kuruhusu hata darasa la Saba kuingia chuo kikuu, ufaulu ukiwa mdogo hapo mwakani Wizara ya Elimu inaweza kunikiza ufaulu ushushwe ili kuwe na wanafunzi wengi wa kujaza vyuo vikuu.
 
viwango viwekwe kuanzia mtoto anapojiunga darasa la kwanza kisha viwango vya kuingia darasa la tano na hivohivo hadi ngazi za juu. hii itaongeza uwajibikaji tangu ngazi za chini kabisa. tatizo viwango vinawekwa juu huku wanafunzi wenye uwezo mdogo kule msingi wakipandishwa ngazi bila kuzingatia viwango madhubuti. wanafunzi wengi wanaoingia kdt cha kwanza wana uwezo mdogo sana wa kumudu masomo
 
watanzania tuache kulalamika hata katika mambo ya maana, ni bora ukawa na wasomi wachache wenye uelewa mzuri na akili nyepesi kuliko kuwa na lundo la wasomi wasiojitambua. namna ya kupata wasomi wazuri ni pamoja na kuongeza kiwango cha ufaulu. anayetaka kwenda chuo anapaswa ajishugulishe sana kusoma na sio kulalama.
 
1.Wanafunzi kuendelea kufeli
2. Viwango vya madaraja ya Ufaulu kuongezeka.
3. Kufikiria kuwapeleka wahitimu wa darasa la saba 'Chuo kikuu'.
4. Kuunda "kikundi kazi" na Tume kuchunguza kufeli kunakoendelea.

With all this, itafika hatua kwenda shule kutakuwa optional! Serikali inatamba kwa kusema Wizara ya Elimu hupata fungu kubwa katika bajeti, ikidhani fedha ni mikakati!

With poor strategic plans, being deaf to Teachers' demands, kuendeleza siasa, kutalimaliza Taifa...Hebu tupige picha mbele (imagine), miaka 15 hadi 20 ijayo, Taifa litakuwa na wasomi? Maana hawa wanaofeli katika miaka hiyo ndio watakaokuwa viongozi, wazazi, walezi!
 
elimu ya secondary sijui imeingiwa na mdudu gani kwa ipindi cha miaka hii michache mbona enzi za mwalimu hadi mkapa haya madudu hayakuwepo?? jibu ni kwamba watu wanaamka huko kwao anakuja na wazo la kubadili kitu fulani bila kufanya utafiti wa kina kupata mazingira halisi ya kubadilisha kitu husika na hii italipeleka pabaya sana taifa hili kielimu.
 
hehehe mungu ndie mjuzi zaid...Sipati picha miaka 15 ijayo hali ya umbumbumbu hapa nchini ita'rise kwa kiwango gani!its just the matter of time!:amen:
 
Hii habari imepingwa vikali sana, tena sana na NECTA. Hata kwenye toleo la Raia Mwema (la kwenye mtandao) kuna hiyo habari; habari hiyo inahusiana na kufeli kwa Kidato cha Nne, 2012.

Mkuu labda wameamua kupingana na majibu ya tume waliyoiunda wao wenyewe baada ya matokeo mabaya ya kidato cha 4 mwaka 2010,
Pia jiulize kwanini safari serkali imeshusha wasifu wa kujiunga na A-level ambapo watachukua wenye C 2 na D pass 3? Badala ya C 3 kama ilivyozoeleka huko nyuma? Pia hujiulzi kwann waziri anasisitiza kuwa hata mwanafunzi mwenye C 2 na D pass 3 ana uwezo na sifa za kujiunga na Alevel? Hii ni kwa sababu wanatambua fika ni jinsi gani wanavyomark mitihani kwa kutumia alama za juu thus y wanatoa go ahead.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…