msemakweli Tanganyik
Member
- Apr 5, 2013
- 18
- 3
Ndugu wana JF wakati huu ambapo jamii ya watanzania wameduaa wasijue cha kufanya baada ya mshtuko wa kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka jana ambapo hata jawabu la tatizo hilo bado linatafutwa na serikali kwa kuunda hata tume za uchunguzi,Baraza la mitihani (NECTA) limeongeza viwango vipya vya ufaulu kwa wanafunzi walio kidato cha sita sasa hivi.Swali ninalo jiuliza ambalo katika hali ya kawaida lilitakiwa kujibiwa na mwendeshaji wa mitaala (curricular developer) je kumekuwa na ufaulu mkubwa sana kwa wanafunzi hawa kiasi cha kufikiria kuwa wanafunzi wanapata alama za ufaulu kwa urahisi bila bidii inayotakiwa? au ni kutuandalia sisi wananchi kilio kingine mwaka kesho? je kwa nini swala la Elimu linakuwa rahisi kuibuliwa na kutekelezwa kiasi hiki? je watendaji wanajua haya ni maamuzi nyeti yanayohusu maisha ya watanzania wengi?.Mfano wa swala hili kuliona wanalifanyia mzaha ni pia katika kudahili wanafunzi ambako walioko kidato cha sita sasa hivi awali walielewa kuwa watafanya mitihani yao mwaka kesho mwezi wapili kama ilivyokuwa kawaida.Ghafla wamebadilishiwa utaratibu na sasa mitihani hiyo wataifanya mwezi wa tano mwaka kesho.Je kwanini hili halikufahamika tangu mwanzo?