Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 355
- 486
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania !
Chama cha mapinduzi ni miongoni mwa vyama vya siasa vilivyopata bahati kubwa sana ya kuwa na tunu ya watu wenye uwezo na weledi mkubwa sana linapokuja suala la uongozi na utawala. hii sio mara ya kwanza kwa jambo hili kuzungumzwa lakini, nitajaribu kuzungumza kwa kadri nionavyo mimi pamoja na uzoefu wangu katika kupekuapekua haya mambo ya kimedani.
Awamu ya kwanza iliyoongozwa na muasisi wa taifa letu Hayati Mwalimu, Julius Nyerere ndio msingi wa mambo yote mazuri tunayoyaona leo, jitihada zake katika ujenzi wa taifa zimekuwa ni wimbo kwa wanasiasa wa leo karibia wote. Umoja na mshikamano bila kujali dini, rangi, kabila wala kipato cha mtu vimekuwa chachu ya amani katika taifa letu kwa takribani miaka sitini na tatu sasa.
Haina ubishi kwamba bila amani hakuna jambo lolote la kimaendeleo linaweza kufanyika, ndio kusema kwamba, amani tunayoifaidi leo ni, zao la mawazo ya mwanaccm huyo kwani, kuunganisha makabila 120 yawe kitu kimoja sio jambo la kuchukulia rahisi hata kidogo, wenzetu wanamakabila machache lakini wameshindwa.
Kwa kutambua mchango wa awamu zote tano zilizopita, moja kwa moja tuangazie hadi awamu ya sita chini ya Rais Samia,.
Rais Samia Hassan ni kiongozi wa aina yake tunaepaswa kujivunia kama taifa. Upole wa sura yake uliwadanganya maadui zake wa kisiasa wakidhani kwamba angekuwa mpole vilevile hata katika uwanja wa mapambano ya kisiasa, matokeo yake kumbe walitaka kucheza na chui jike kama alivyowahi kujiita hapo nyuma. Viwango anavyovitumia kuliongoza taifa ni viwango vya aina yake.
Nitajaribu kuelezea ni kwa namna gani Rais Samia amekuwa ni rais mwenye viwango vya aina yake katika upande wa siasa.
Kwanza ni uthubutu wake katika kuimarisha demokrasia ya Tanzania.
Hili alianza kulionesha mara tu alipoapishwa kuwa rais wa taifa letu, hakika kwa joto la siasa lililokuwepo wakati ule na uamuzi aliochukua, kila mtu alingoja kwa hamu kuona nini kinaendelea.
Ndio kusema kwamba, kufuatia maoni ya wadau wa demokrasia waliokutana jijini Dodoma kati ya tarehe 15-17 desemba 2021, kiliundwa kikosi kazi kilichoongozwa na profesa Mukandala kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, lengo likiwa ni kwenda kuangazia pembe muhimu za kugusa ili kuboresha mazingira ya kisiasa nchini.
Moja ya mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi hicho tarehe 21 oktoba 2022 , ni pamoja na kuruhusu mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa, kikosi kazi kilisisitiza kuwa shughuli hizo za kisiasa zifanyike bila vikwazo vyovyote. Ni tofauti na hali ilivyokuwa miaka michache nyuma kabla ya Rais Samia kuingia madarakani.
Baada ya hapo sote tumekuwa mashahidi kwamba wapinzani sasa wanafanya shughuli zao bila bughudha za kiutawala, tumeshuhudia maandamano ya amani na operesheni mbalilmbali za vyama vya siasa. Na wengine hata kujisahau kutumia majukwaa hayo kumdhihaki yeye kama Samia na sio yeye kama Rais, hii yote ni furaha iliyoletwa na rais Samia kwa wanasiasa wa upinzani.
Kimsingi ni kuwa, madongo yanayorushwa kwa Rais Samia ni mengi na makubwa mno, nina uhakika kabisa angekuwa ni raisi mwingine yeyote yule (hata mimi) ningezuia mara moja upenyo huo kwani bila kuwa imara unaweza kutoka kwenye reli bila utambuzi. Maajabu ni kwamba licha ya madongo na makelele tunayoyaona na kuyasikia, Rais Samia hajaonesha kuteterereka, ndo kwanza nchi anaijenga na anaendelea kujipatia kibali cha kuwaongoza watanzania tena hapo itakapofika 2025.
Hakika kiwango hiki cha uvumilivu ni kikubwa sana na tunaweza kusema sio tu kuiongoza Tanzania bali Samia anailea Tanzania, Samia ni mama, Samia ni mama wa taifa.
Ni kwa sababu ya ruhusa hiyo ya mikutano ya vyama vya siasa, chuki na uhasama mkubwa wa kisiasa umepungua.
Pili ni uthubutu wake katika kuimarisha sera ya usawa wa kijinsia katika siasa.
Bila kuathiri sera ya usawa wa kijinsia, kikosi kazi kimeeleza wazi kuwa ni lazima shughuli za kisiasa ziende sambamba na usawa wa kijinsia, ndio kusema kwamba, litakuwepo sharti la lazima kwa kila chama cha siasa kuwa na sera ya usawa wa kijinsia na kuhakikisha kwamba idadi ya jinsia moja katika vyombo vya maamuzi ndani ya chama isipungue asilimia arobaini. hii ndiyo Tanzania anayoitaka Samia na tunayoitaka watanzania.
Hebu fikiria, mtu hayupo tayari aidha kupeleka mtoto wa kike shule, hayupo tayari kuona mwanamke akishika uchumi na hayupo tayari kuona mwanamke akishika nafasi za uongozi, kakini mtu huyohuyo muulize hivi ; hupendi mama yako awe rais kama Samia?, hupendi mwanao awe na pesa aje kukusaidia? hupendi binti yako awe spika kama tulia?, mtu huyo atakujibu kwa bashasha kuwa angependa ! kwahio ni ujinga tu uliopo kwenye vichwa vya waliowengi,
hivyo kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na kikosi kazi tutegemee dada zetu, wadogo zetu na mama zetu wakionekana kuwa mstari wa mbele katika siasa za Tanzania. Hili si jambo la kubeza, ajenda ya usawa wa kijinsia ni ajenda ya kimataifa. Mheshimiwa Rais ni wa viwango vya kimataifa na uchaguzi mkuu 2025 atawanyoa wapinzani kwa chupa.
Tatu ni uthubutu wake wa kuonesha nia ya kufufua mchakato wa katiba mpya.
Kihistoria katiba mpya sio jambo linaloweza kupatikana kwa wepesi. hata hivyo pamoja na ukweli kwamba wanaohitaji katiba mpya sio wananchi bali sehemu tu ya wanasiasa na kwa maslahi yao binafsi, mheshimiwa rais ameonesha nia ya kufufua mchakato huo, kimsingi ikipatikana haitanufaisha hao wanasiasa peke yao bali taifa zima kwa ujumla wake.
Lakini pia licha ya imani yao kuwa katiba mpya ndiyo itawasaidia kumuondoa madarakani kwa wepesi, Rais Samia haoneshwi hata kuogopeshwa na ndo kwanza kazi inaendelea, hii maana yake ni kwamba katiba mpya sio suluhisho kwa wapinzani kuingia chamwino house bali ni nia thabiti ambayo wananchi wa jamhuri ya muungano wataiona kwa mgombea, sisi wananchi tunamuona Samia kuwa na nia hiyo.
Imani na nia ya kufufua mchakato wa katiba mpya bila machafuko ya kuandaliwa ni jambo lililompa Rais Samia mtaji mkubwa sana wa kisiasa, hii inamaanisha kuwa chui jike huyu ndiye atakaekuwa mgombea mwenye viwango vya hali ya juu zaidi kuliko wagombea wengine kati ya wagombea wa urais wa mwaka 2025.
Kwa kumaliza tu, uimarishaji wa demokrasia nchini kwa kuruhusu shughuli za kisiasa bila bughudha, kuimarisha sera ya usawa wa kijinsia ndani ya vyama na nje ya vyama vya siasa pamoja na nia ya kufufua mchakato wa katiba mpya, ni mambo makuu matatu ambayo yamempa thamani ya hali ya juu ya kisiasa Rais Samia, ikiwa na maana kuwa amepanda viwango zaidi, kupanda viwango kwa Rais Samia ni ishara kuwa CCM itashinda kwa kimbunga katika uchaguzi mkuu wa hapo mwakani 2025.
Asante na Kazi Iendelee.
Yusufu R H Sabura
0750883466/0717934194.