Tlmau
Member
- May 12, 2019
- 11
- 14
Habari,naitwa Titus Devis.. karibu sana tuongee kuhusu viwango vya riba au interest rate kwa lugha ya kigeni
Kwanza kabisa tuanze na viwango vya riba ni nini (what is interest rate)
-Viwango vya riba ni kiasi cha pesa ambacho kinaongezeka kwenye pesa ambayo mkopaji amekopa baada ya muda Fulani na mara nyingi hizi riba huwa huwa zinapagwa kwa mfumo wa asilimia(%),riba zitokanazo na mikopo kitaalamu huwa zinafahamika Kama annual percentage rate(APR).
Viwango vya riba hutumika kwa mtu ambae ni mkopaji,mkopaji huyu anaweza kukopa pesa kwa ajili ya kununua nyumba,kuendeleza biashara,kulipia ada na mambo mengine mengi sana. Moja Kati ya vitu vya kuwa navyo makini sana kabla ya kukopa ni kufahamu vizuri viwango vya riba kutokana na mkopo unaotaka kuuchukua kwa sababu utakusaidia kujua Kama riba inakuumiza au laa,pia utakusaidia kujua kutokana na riba uliyonayo utalipa mkopo wako kwa muda gani kutokana na muda mabao mmekubaliana kulipana mkopo wenu
Mfano wa viwango vya riba,Kama utakopa 1000,000 kutoka bank na ukaambiwa riba yake ni 10% maana yake mwisho wa siku utatakiwa kulipa milioni moja na laki moja ili kumaliza mkopo wako (10÷100)×1000,000=100,000
100,000 ya riba +1,000,000 ya mkopo wako jumla inakua 1,100,000
Natumaini umenipata.
Kitu ambacho inabidi ufahamu ni kwamba mabadiliko ya viwango vya riba katika nchi husika viko chini ya benki kuu (central banks) mfano Tanzania tuna B.O.T ambayo ndo inahusika kutengeneza sera mbalimbali za kifedha nchini (monetary policy), sera za fedha huwa zinabadilika kutokana na sababu mbalimbali ili kuimarisha uchumi katika wakati husika ili kubalance shughuli mbali mbali za kiuchumi nchini mfano ili kufanya usawa wa kibiashara (trade balance),kucontrol mlipuko wa Bei (inflation) n.k
Mfano mzuri ni kipindi cha pandemic Kama Tsunami,matetemeko,magojwa Kama ilivo korona nk kwasababu vitu Kama hivi huwa na athari kwenye uchumi wa nchi husika bank kuu huwa inalazmika kubadilisha mfumo wa sera za kifedha ili kuendana na hali ya muda huo,
Nchi Kama USA kipindi covid 19 imepanda Moto walifanya kitu kunaitwa stimulus (wanaprint pesa na kuzitawanya kwenye biashara kwa utaratibu maalumi ili ku support biashara zisife kabisa na hii ilisaidia sana baadhi ya biashara kutopotea kipindi hicho ambacho uchumi ulikua na hali mbaya sana duniani nadhani wote tunalijua hili na kwakufanya hivi maana yake Kuna baadhi ya watu waliendelea kufanya kazi kwenye hizo company zilizonufaika na Kodi waliipa,tayar serikal ilikua inaendelea kupata mapato japo yalikua kidogo sana kwa sababu nguvu ya ununuzi kutoka kwa raia ilipungua sana kutokana na lockdown
-Turudi kwenye agenda yetu sasa(ongeza popcorn 😃)
Mwezi wa tano(2021) Kama nakumbuka vizuri banki kuu ya Tanzania ilipunguza viwango vya riba kwa asilimia Fulani mfano viwango vilikua ni 4% alafu vipunguzwe hadi 2.6% hii maanya yake nini?
Fahamu kwamba benki kuu ndo huwa inatoa mokopo kwa hizi local banks zetu Kama crdb,nmb nk. Hivo basi Kama B.O.T wakipunguza viwango vya riba maana yake pia local banks zitachukua mikopo ya riba nafuu kutoka benki kuu ili kuendeshea shughuli mbalimbali za kibenki,Kama ilivo kwenye familia baba akicheka basi familia yote inafurahi,hivo basi hata kuku ni hivo hivo Kama local banks zimechukua mkopo kwa riba ndogo maana yake hata wewe mwananchi wa kawaida au taasisi binafsi au ya serikali itakuchukua mikopo ambayo ina riba nafuu na sio kama ilivokua mwanzo, mfano Kama bank ilikua inatoa riba ya 15% kwa mkopo wa tsh 1000,000 Kuna uwezekano mkubwa riba hiyo ikashuka hadi 10% labda.
Hii huwa ni furaha kwa wafanya biashara kwa sababu wanakua na uwezo wa kuchukua mikopo yenye riba nafuu ili kuendeleza biashara zao,na biashara zikifanikiwa maana yake wafanya biashara watalipa kodi na pia watatoa ajira kwa kwa wananchi na hivo kupelekea pato la taifa kukua (GDP growth) na ndio maana nchi Kama USA zinawasaidia sector binafsi kuendelea kwasabu wanajua hizo sector zikifanikiwa ni utajiri kwa nchi kweye nyanja mbalimbali.
#japokua hii habari ya kupungua kwa rates huwa sio nzuri sana kwa wawekezaji wan ndani na nje ya nchi kwa sababu wanakua marejesho yao yatakua madogo katika investment ambazo wamewekeza au wanataka kuwekeza katika nchi husika.
Najua uzi mtamu😄,tumalizie sasa
Nini itatokea endapo hizi central banks zitaongeza viwango vya riba,Kama kawaida ni kinyume cha hapo juu (japokua siku nyingine tutaongea vizuri vitu gani vinasababisha benki kuu kuongeza viwango vya riba). Sasa Kama benki kuu itaongeza viwango vya riba maana yake hata hizi local banks zetu zitapandisha riba zao na Kama tunavojua riba kubwa huwaga sio rafiki kwa wengi wetu iwe mtu binafsi au hata biashara fulani, kitu ambacho kinapelekea biashara nyingi hasa ndogo kudumaa na zingine kufa kabisa kutokana na kutokukidhi fedha za kuendesha biashara hizo na kupelekea hata ajira kupotea kitu kinachofanya hata serikali kukosa mapato kwa sababu ya upungufu wa kodi.
Asante kwa wewe ambae umesoma huu uzi natumaini utakua umejifunza kitu. Mungu akubariki na uwe na siku njema.
#zingine nyingi zitafuta
#usisahau kuvote