Viwango vya wachezaji kwenye Derby ya 23.10.2022

Viwango vya wachezaji kwenye Derby ya 23.10.2022

Vawulence

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2009
Posts
1,930
Reaction score
2,118
Kwa kuzingatia utendaji na michango ya wachezaji, hapa nitajaribu kutumia kipimo cha 1-10 kiwafanyia viwango wachezaji wa timu zote mbili.

Simba:

1. Aishi Manula 7.5
Alifanya kazi kubwa ya kuokoa hatari na pia kuanzisha mipango ya timu. Uzoefu wake ulisababisha kupatikana goli la Simba. Hata hivyo ameonesha kuwa vulnerable kwa kushindwa kupanga ukuta hadi akafungwa.

2. Mohamed Hussein 7.8
Alikuwa na kiwango kizuri sana. Alikuwa akipandisha mashambulizi na kukaba nafasi kwa ufanisi. Kisinda alionekana wa kawaida sana.

3. Israh Mwenda 7.5
Alifanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Kutokana na umri wake mdogo inaonesha atakuwa bora na hata kumuweka Kapombe benchi. Anatakiwa kuongeza umakini na kasi ya kuachia mipira.

4. Enock Inonga 7.4
Aliweza kuzuia njia lakini alikuwa akipoteza pasi nyingi kwa kupiga mipira bila umakini.

5. Onyango 7.8
Alikuwa na siku nzuri kazini. Umakini mkubwa kwa mipira ya juu na kumnyima pumzi Mayele. Alikuwa mzito kukimbia ila alitumia akili nyingi kurekebisha makosa yake na ya wenzake haraka.

6. Mzamiru Yassin 8.2
Alikuwa na kazi kubwa ya kufanya. Alifanya kazi kubwa ya kiungo mkabaji akijitahidi kusahihisha makosa ya Mkude aliyeonekana kutoendana na mchezo. Alistahili kuwa Man of the match kwa upande wangu.

7. Jonas Mkude 5.7
Alifanya makosa mengi na hakuendana na kasi ya mchezo. Kama refa angekuwa makini basi alostahili kadi nyekundu kwa uzembe kabisa.

8. Clatous Chama 7.8
Alionesha kuwa ni mchezaji wa kimataifa na ana uwezo wa kucheza bila presha hata kwenye mechi ngumu. Assist aloyotoa kwa Okrah anaweza kutoa yeye pekee yake kwenye ligi yetu. Bila shaka atakuwa MVP wa 2022/2023.

9. Sakho 6.0
Alionesha kiwango kizuri lakini bado ana tatizo la kukaa na mpira muda mrefu na kutoa pasi sehemu isiyo sahihi. Bado ana utoto mwingi.

10. Moses Phiri 5.4
Hakuwa na siku nzuri kazini. Alikuwa na wakati mgumu kwa Bangala na Job. Alifanikiwa kupiga faulo 1 tu tena nje ya lango. Alikuwa msaada mkubwa akirudi nafasi ya kiungo kumsaidia Mkude mara kwa mara.

11. Augustine Okra 9.2
Man of the match. Aliwanyima mabeki wa Yanga raha muda wote. Kama refa angekuwa makini basi Okrah angepelekea wachezaji Djuma na Aucho kula umeme. Alionesha dhahiri umri wa Djuma umeenda sana.

12. Habib Kyombo 6.2
Anaonesha ana uwezo mkubwa sana na anaweza kuwa mshambuliaji hatari wa Kitanzania kama akipewa muda zaidi. Alliweza kuwin mipira yote ya juu katikati ya mabeki. Kwa muda mfupi aliocheza alikuwa na impact kubwa sana.

13. Kibu Denis 4.6
Inaonesha kuna jambo haliko sawa kwake. Ana nguvu, kasi na uwezo wa kukokota mpira ila anafeli sana upande wa kufanya maamuzi sahihi. Kwa siku za mbeleni naona wazi akikosa namba na kutolewa kwa mkopo kabla msimu haujaisha.

14. Erasto Nyoni 4.6
Aliingia dakika za majeruhi kabisa.

YANGA

1. Dijgu Diarra 7. 2

Alikuwa mzuri golini ila alifanya baadhi ya makosa ambayo huenda yangezalisha magoli zaidi.

2. Djuma Shabani 6.7
Alikuwa na wakati mgumu sana kukabiliana na Okrah. Alithibitisha maneno ya Zahera kuwa amenenepa sana. Alikuwa na uoga wa kupanda kusaidia kujenga mashambulizi kama kawaida yake.

3. Kibwana Shomari. 7.0
Anapoteza kujiamini, amekuwa na uoga wa kupandisha mashambulizi lakini pia winga wake Kisinda hakuwa akimsaidia kurudi kukaba nafasi timu ikipoteza mpira.

4. Dickson Job 7.2
Alicheza kwa umakini mkubwa sana. Alidhihirisha kuwa akizidi kuaminiwa atakuwa bora sana. Kukosa mawasiliano mazuri na golikipa wake kulikaribia kuiadhibu timu.

5. Yanick Bangala 7.0
Alielemewa sana na mashambulizi. Kushindwa kwake kumfanyia marking Okrah kulisababisha kufungwa. Pia alikuwa na wakati mgumu sana alipoingia Kyombo. Hakuweza kuwin mpira wowote dhidi ya Kyombo.

6. Khalid Aucho 6.4
Alishindwa kukamata dimba kabisa na pia uzito mkubwa ama majeruhi yanamfanya kokosa kasi na kufanya makosa ya hatari. Uzoefu wake ulisaidia kupata faulo iliyozaa goli zuri la Ki Aziz. Alistahili kadi nyekundu kwa makosa ya kujirudia.

7. Feisal Salum 6.8
Alijitahidi kukamata dimba la Kati lakini Mzamiru Yasin alimdhibiti vilivyo. Bado ana tatizo la kushindwa kufanya maamuzi kwa wakati sahihi.

8. Moloko 5.5
Ameonesha ni mchezaji wa kawaida sana. Alidhibitiwa vilivyo na Israh Mwenda. Ana kasi nzuri lakini anakosa malengo. Hakuweza kusababisha hatari yoyote kwenye lango la mpinzani.

9. KI Aziz 7.0
Zaidi ya goli alilofunga hakuwa na maajabu kabisa. Alidhibitiwa vilivyo na Mzamiru na onyango. Anakokota mpira muda mrefu hadi anapoteza. Hawezi kusaidia timu ikiwa haina mpira.

10. Fiston Mayele 6.7
Licha ya kutokufunga goli anabakia kuwa mchezaji hatari sana. Inaonesha alipigwa "Misumari" akawa anshindwa kutumia nafasi vyema. Alikuwa akirudi kati kutafuta mpira na kusaidia kukabia juu.

11. Tuisila Kisinda 4.6
Zaidi ya mbio hana cha kuipatia timu kabisa. Anakosa uwezo wa kushikilia mpira mpaka wenzake wafike mwenye nafasi. Anacheza traditional football anaenda mbele tu hata kama hakuna uwezekano wa kupita. Siyo mzuri off ball.

12. Farid Musa 6.2
Nashindwa kuelewa ni kwa nini Nabi anashindwa kumuamini. Alipoingia aliweza kumtingisha Onyango na kama angekuwa makini wangepata goli. Ana kasi nzuri, anashikilia mpira na anajua kucheza kwa nafasi.

13. Gael Bigirimana 4.0
Mpaka sasa najiuliza ni kwanini aliingia uwanjani. Zaidi ya rafu aliyocheza sikumbuki kama aligusa tena mpira. Ni mchezaji mwenye jina kubwa kuliko uwezo.

Mchezo ulikuwa mzuri na wenye presha kubwa sana kwa timu zote mbili.

Muamuzi alijitahidi sana kwa uwezo wake lakini alitoa kadi za njano zisizo na msingi na ambazo zilimpa wakati mgumu kufanya maamuzi kwenye makosa makubwa zaidi

Anapaswa aelewe kuwa refarii mzuri sio anayekuwa mkali kwa wachezaji bali anayekuwa fair na kufanya mamuzi yasiyoleta maswali.

Hayo ni maoni yangu na haimaanishi lazima yawe kama ya kwako.

20221023_162709.jpg
20221024_231214.jpg
 
Yani Mayele ana 6.7 kumzidi Farid Mussa kweli?

Au kwakua kacheza dakika nyingi?

Lakini hizo dakika nyingi alizocheza alizitumia kufanya nini cha maana?

Au ni ile header ya off target?

Hata Baraka Mpenja alikuwa anaona aibu kumita Game changer. Utamuitaje game changer kwenye game kama ya jana na watu wakakuelewa?

Mi nilianza kujua Mayele yupo baada ya Farid Musa kuingia. Huyu ndio mchezaji ambaye nilimuona amekuja na plan ya kimageuzi.

Ila yule mwenye bleach kichwani kama kinyambe sidhani kama anastahili hata hiyo 4.6

Azizi Ki umemuwekea namba kubwa sana (hata yeye akisoma atashangaa), rate yako imejikita kwenye goli na sio perfomance.

Niamini, lile goli lingefungwa na mchezaji mwingine leo hii Bigirimana angeonekana bora kuliko yeye.

Moses Scars Phiri hujamtendea haki (sijapenda) walau ungem bust hata kwenye 6 Huko na ushee kuliko kumuweka level za kina Moloko

Huyu jamaa ukiacha Ile role yake ya kushambulia ila jana alikuwa anapokonya na mipira, jambo ambalo huwezi kulikuta kwa Mayele.

Israh mwenda na Zimbwe hawa ndio sababu ya kumfanya Tuisila aonekane hana kitu.

Aish Manula alikuwa kwenye kiwango bora, goli alilofungwa lilikuwa gumu kuweza ku save.

Ni goli zuri lazima tumpe credit mfungaji (ila asijisahau) sioni sehemu yeyote ya kumpa lawama Manula

Mwisho natoa rate yangu kwa Ramadhani Kayoka nampa 9/10 kwa kuharibu game ya jana.

Alitoa kadi nyingi za njano mwanzoni mwa mchezo kiasi kilichomfanya aogope kutoa kadi ya pili ya njano ambayo ingekuwa ni direct red card kwa wachezaji waliorudia kufanya makosa

Faulo ya Feisal kwa Kyombo ilikuwa ni faulo iliyomhitaji kutoa kadi ya njano ambapo ni red card kutokana na kwamba alishaonywa kwa kadi ya njano kabla.

Lile kwangu lilikuwa ni shambulizi lenye kukupa 85% ya uwezekano kupata goli, Yanga wanaweza kuona wachezaji flani flani wamecheza vizuri ila kwa kitendo hicho Cha Feisal inabidi wampongeze sana kwa kuinusuru timu
 
Yani Mayele ana 6.7 kumzidi Farid Mussa kweli?

Au kwakua kacheza dakika nyingi...
Nakubaliana na wewe 100% rating yangu imezingatia zaidi kazi aliyopaswa kufanya mchezaji na ufanisi wake. Feisal alichofanya ndio ambacho huwa anafanya Putin.

Anamalizana na adui ili kupunguza ukali wa mashambulizi. Hata akipata kadi inakuwa ameshaokoa timu.
 
Hakuna mchezaji wa kumrate 9 kwenye Mechi mbovu kama Ile labda kama unafanya Love rating.
Mimi sijafanyia mechi rating bali nimefanyia mchezaji mmoja mmoja. Na pia hata mechi ikiwa mbovu namna gani kuna wachezaji watakuwa na rate kubwa zaidi ya wengine.

Kwa mfano mechi ya Zalan vc Yanga yule golikipa lazima umpe rating kubwa kuliko Mshery maana aliokoa hatari nyingi kuliko magoli aliyofunga.
 
Mimi sijafanyia mechi rating bali nimefanyia mchezaji mmoja mmoja. Na pia hata mechi ikiwa mbovu namna gani kuna wachezaji watakuwa na rate kubwa zaidi ya wengine...
Mimi nimekwambia Hakuna Mchezaji wa kumrate 9 out of 10. Hata kama ni mapenzi muwe mnaongea uhalisia siyo kusombwa na ufurukutwa.

Umemrate mchezaji 9.2 Kwamba madhaifu yake yalikuwa 0.8 pekee? Siyo huyu Kila shabiki wa Simba anamlaumu Kwa maamuzi mabovu zaidi ya x5?
 
Kwa kuzingatia performance na contribution ya wachezaji hapa nitajaribu kutumia scale ya 1-10 kiwafanyia rating wachezaji wa timu zote mbili.

SIMBA:

1. Aishi Manula 7.5
Alifanya kazi kubwa ya kuokoa hatari na pia kuanzisha mipango ya timu. Uzoefu wake ulisababisha kupatikana goli la Simba. Hata hivyo ameonesha kuwa vulnerable kwa kushindwa kupanga ukuta hadi akafungwa.

2. Mohamed Hussein 7.8
Alikuwa na kiwango kizuri sana. Alikuwa akipandisha mashambulizi na kukaba nafasi kwa ufanisi. Kisinda alionekana wa kawaida sana.

3. Israh Mwenda 7.5
Alifanya kazi kwa weledi wa hali ya juu. Kutokana na umri wake mdogo inaonesha atakuwa bora na hata kumuweka Kapombe benchi. Anatakiwa kuongeza umakini na kasi ya kuachia mipira.

4. Enock Inonga 7.4.
Aliweza kuzuia njia lakini alikuwa akipoteza pasi nyingi kwa kupiga mipira bila umakini.

5. Onyango 7.8
Alikuwa na siku nzuri kazini. Umakini mkubwa kwa mipira ya juu na kumnyima pumzi Mayele. Alikuwa mzito kukimbia ila alitumia akili nyingi kurekebisha makosa yake na ya wenzake haraka.

6. Mzamiru Yassin 8.2
Alikuwa na kazi kubwa ya kufanya. Alifanya kazi kubwa ya kiungo mkabaji akijitahidi kusahihisha makosa ya Mkude aliyeonekana kutoendana na mchezo. Alistahili kuwa Man of the match kwa upande wangu

7. Jonas Mkude 5.7
Alifanya makosa mengi na hakuendana na kasi ya mchezo. Kama refa angekuwa makini basi alostahili kadi nyekundu kwa uzembe kabisa

8. Clatous Chama 7.8
Alionesha kuwa ni mchezaji wa kimataifa na ana uwezo wa kucheza bila presha hata kwenye mechi ngumu. Assist aloyotoa kwa Okrah anaweza kutoa yeye pekee yake kwenye ligi yetu. Bila shaka atakuwa MVP wa 2022/2023

9. Sakho 6.0
Alionesha kiwango kizuri lakini bado ana tatizo la kukaa na mpira muda mrefu na kutoa pasi sehemu isiyo sahihi. Bado ana utoto mwingi.

10. Moses Phiri 5.4
Hakuwa na siku nzuri kazini. Alikuwa na wakati mgumu kwa Bangala na Job. Alifanikiwa kupiga faulo 1 tu tena nje ya lango. Alikuwa msaada mkubwa akirudi nafasi ya kiungo kumsaidia Mkude mara kwa mara..

11. Augustine Okra 9.2
Man of the match. Aliwanyima mabeki wa Yanga raha muda wote. Kama refa angekuwa makini basi Okrah angepelekea wachezaji Djuma na Aucho kula umeme. Alionesha dhahiri umri wa Djuma umeenda sana.

12. Habib Kyombo 6.2
Anaonesha ana uwezo mkubwa sana na anaweza kuwa mshambuliaji hatari wa Kitanzania kama akipewa muda zaidi. Alliweza kuwin mipira yote ya juu katikati ya mabeki. Kwa muda mfupi aliocheza alikuwa na impact kubwa sana.

13. Kibu Denis 4.6
Inaonesha kuna jambo haliko sawa kwake. Ana nguvu, kasi na uwezo wa kukokota mpira ila anafeli sana upande wa kufanya maamuzi sahihi. Kwa siku za mbeleni naona wazi akikosa namba na kutolewa kwa mkopo kabla msimu haujaisha.

14. Erasto Nyoni 4.6
Aliingia dakika za majeruhi kabisa.

YANGA

1. Dijgu Diarra 7. 2

Alikuwa mzuri golini ila alifanya baadhi ya makosa ambayo huenda yangezalisha magoli zaidi.

2. Djuma Shabani 6.7
Alikuwa na wakati mgumu sana kukabiliana na Okrah. Alithibitisha maneno ya Zahera kuwa amenenepa sana. Alikuwa na uoga wa kupanda kusaidia kujenga mashambulizi kama kawaida yake.

3. Kibwana Shomari. 7.0
Anapoteza kujiamini, amekuwa na uoga wa kupandisha mashambulizi lakini pia winga wake Kisinda hakuwa akimsaidia kurudi kukaba nafasi timu ikipoteza mpira.

4. Dickson Job 7.2
Alicheza kwa umakini mkubwa sana. Alidhihirisha kuwa akizidi kuaminiwa atakuwa bora sana. Kukosa mawasiliano mazuri na golikipa wake kulikaribia kuiadhibu timu.

5. Yanick Bangala 7.0
Alielemewa sana na mashambulizi. Kushindwa kwake kumfanyia marking Okrah kulisababisha kufungwa. Pia alikuwa na wakati mgumu sana alipoingia Kyombo. Hakuweza kuwin mpira wowote dhidi ya Kyombo.

6. Khalid Aucho 6.4
Alishindwa kukamata dimba kabisa na pia uzito mkubwa ama majeruhi yanamfanya kokosa kasi na kufanya makosa ya hatari. Uzoefu wake ulisaidia kupata faulo iliyozaa goli zuri la Ki Aziz. Alistahili kadi nyekundu kwa makosa ya kujirudia.

7. Feisal Salum 6.8
Alijitahidi kukamata dimba la Kati lakini Mzamiru Yasin alimdhibiti vilivyo. Bado ana tatizo la kushindwa kufanya maamuzi kwa wakati sahihi.

8. Moloko 5.5
Ameonesha ni mchezaji wa kawaida sana. Alidhibitiwa vilivyo na Israh Mwenda. Ana kasi nzuri lakini anakosa malengo. Hakuweza kusababisha hatari yoyote kwenye lango la mpinzani.

9. KI Aziz 7.0
Zaidi ya goli alilofunga hakuwa na maajabu kabisa. Alidhibitiwa vilivyo na Mzamiru na onyango. Anakokota mpira muda mrefu hadi anapoteza. Hawezi kusaidia timu ikiwa haina mpira.

10. Fiston Mayele 6.7
Licha ya kutokufunga goli anabakia kuwa mchezaji hatari sana. Inaonesha alipigwa "misumari" akawa anshindwa kutumia nafasi vyema. Alikuwa akirudi kati kutafuta mpira na kusaidia kukabia juu.

11. Tuisila Kisinda 4.6
Zaidi ya mbio hana cha kuipatia timu kabisa. Anakosa uwezo wa kushikilia mpira mpaka wenzake wafike mwenye nafasi. Anacheza traditional football anaenda mbele tu hata kama hakuna uwezekano wa kupita. Siyo mzuri off ball.

12. Farid Musa 6.2
Nashindwa kuelewa ni kwa nini Nabi anashindwa kumuamini. Alipoingia aliweza kumtingisha Onyango na kama angekuwa makini wangepata goli. Ana kasi nzuri, anashikilia mpira na anajua kucheza kwa nafasi.

13. Gael Bigirimana 4.0
Mpaka sasa najiuliza ni kwanini aliingia uwanjani. Zaidi ya rafu aliyocheza sikumbuki kama aligusa tena mpira. Ni mchezaji mwenye jina kubwa kuliko uwezo.

Mchezo ulikuwa mzuri na wenye presha kubwa sana kwa timu zote mbili.

Muamuzi alijitahidi sana kwa uwezo wake lakini alitoa kadi za njano zisizo na msingi na ambazo zilimpa wakati mgumu kufanya maamuzi kwenye makosa makubwa zaidi

Anapaswa aelewe kuwa refarii mzuri sio anayekuwa mkali kwa wachezaji bali anayekuwa fair na kufanya mamuzi yasiyoleta maswali.

Hayo ni maoni yangu na haimaanishi lazima yawe kama ya kwako.
Asante Makolo FC.
 
Mimi nimekwambia Hakuna Mchezaji wa kumrate 9 out of 10. Hata kama ni mapenzi muwe mnaongea uhalisia siyo kusombwa na ufurukutwa. Umemrate mchezaji 9.2 Kwamba madhaifu yake yalikuwa 0.8 pekee? Siyo huyu Kila shabiki wa Simba anamlaumu Kwa maamuzi mabovu zaidi ya x5?
Hayo maamuzi mabovu hayazuii kuwa alikuwa kwenye kiwangobora sana. Hata hivyo nilitaka kumpa rate ya 9.8 hayo makosa (actually kosa moja tu la dhahiri) ndio yamefanya nipunguze rating. Ningefanya rating kwa mapenzi hakuna mchezaji wa Yanga angekuwa above 5.
 
Mimi nimekwambia Hakuna Mchezaji wa kumrate 9 out of 10. Hata kama ni mapenzi muwe mnaongea uhalisia siyo kusombwa na ufurukutwa. Umemrate mchezaji 9.2 Kwamba madhaifu yake yalikuwa 0.8 pekee? Siyo huyu Kila shabiki wa Simba anamlaumu Kwa maamuzi mabovu zaidi ya x5?

Mwandishi anaonekana kabisa ni Kolo ,how mchezaji anayelaumiwa kuokosesha timu ushindi una m-rate 9.2

Rating karibia zote ziko biased
 
Mwandishi anaonekana kabisa ni Kolo ,how mchezaji anayelaumiwa kuokosesha timu ushindi una m-rate 9.2

Rating karibia zote ziko biased
Hao wanaomlaumu wanajua alipewa maelekezo ya kufanya nini uwanjani? Kuna yeyote kwenye benchi la ufundi amemlaumu? Au wachezaji wenzake wamemlaumu?
 
Okra alistali 6/10 maana kwa Mchezaji professional Simba ingetoka na magoli matatu kupitia kwako....kafanya ubinafsi nafasi 2 za wazi kabisa.

Ajifunze kwa Chama ni Mchezaji Anayeupiga mwingi na anahitaji timu ipate ushindi kupitia kwa Mchezaji yeyote aliye kwenye nafasi.

Rate zako ukiziangalia kiundani umeegemea upande mmoja.
 
Hao wanaomlaumu wanajua alipewa maelekezo ya kufanya nini uwanjani? Kuna yeyote kwenye benchi la ufundi amemlaumu? Au wachezaji wenzake wamemlaumu?
Wewe unafikiri kila anachofanya Mchezaji uwanjani kapewa maelekezo?
Kuna matukio unatumia akili zako kujiongeza...Mchezaji lazima uwe na uchungu na timu unayoipigania sio kutaka sifa wewe binafsi.
 
Mzamiru Yasin Hawez akawa na Rate ya juu hivyo alicho saidia ni ku cover eneo kubwa la uwanja ila kwenye second ball hakuwa vizuri kwa mkude nakubali

Pia mchezaji hawezi kwenda kucheza dk 15 akapewa rate ya 6 haiwezekani

Aucho na Fei
Aucho upo sahihi kwa mechi kama ile na sio ile Toka aucho arudi kucheza Holding hajawahi kuwa na ufanisi kwa 80%...

Fei kurudi chini kuna ifanya timu isitembee japo kuwa kijana ana jitahidi sana ..

Kwenye mchezo wa Juzi Yanga nikama hawakuwa tayari ku ucheza ule mchezo...

Wachezaji wengi wamecheza chini ya kiwango
Diarra
Mayele
Aucho
Moloko
Azizi K
Kisinda
 
Okra alistali 6/10 maana kwa Mchezaji professional Simba ingetoka na magoli matatu kupitia kwako....kafanya ubinafsi nafasi 2 za wazi kabisa,
Ajifunze kwa Chama ni Mchezaji Anayeupiga mwingi na anahitaji timu ipate ushindi kupitia kwa Mchezaji yeyote aliye kwenye nafasi.
Rate zako ukiziangalia kiundani umeegemea upande mmoja.
Rating za mpira haziko hivyo. Hazifanyiki kwa hisia bali kwa kutazama performance. Kama tutatumia hisia basi aliyesababisha faulo ikazaa goli apate ndogo zaidi. Na sijaegemea upande mmoja. Nindhahiri kuwa Simba walitawala mchezo kuanzia mwanzo mpaka mwisho hivyo wachezaji wake watakuwa na rate za juu kwa vyovyote.
 
Mzamiru Yasin Hawez akawa na Rate ya juu hivyo alicho saidia ni ku cover eneo kubwa la uwanja ila kwenye second ball hakuwa vizuri kwa mkude nakubali

Pia mchezaji hawezi kwenda kucheza dk 15 akapewa rate ya 6 haiwezekani

Aucho na Fei
Aucho upo sahihi kwa mechi kama ile na sio ile Toka aucho arudi kucheza Holding hajawahi kuwa na ufanisi kwa 80%...

Fei kurudi chini kuna ifanya timu isitembee japo kuwa kijana ana jitahidi sana ..

Kwenye mchezo wa Juzi Yanga nikama hawakuwa tayari ku ucheza ule mchezo...

Wachezaji wengi wamecheza chini ya kiwango
Diarra
Mayele
Aucho
Moloko
Azizi K
Kisinda
Sikupingi ila kwa Mzamiru nimejaribu kuangalia kazinkubwa aliyokuwa nayo. Kweli hakuwa mzuri kwenye second balls lakini alijitahidi sana kupressurize mpinzani na kufukia makosa menginya Mkude. Naamini Putin angekuwepo basi Mzamiru kazi yake ingeonekana vizuri maana angekuwa na eneo dogo la kufanyia kazi.

Kyombo alicheza dakika chache lakini alikuwa na impact kuliko Phiri na Saka. Naamini kama angeanza kipindi cha pili angesababisha matokeo yawe tofauti. Nimempa 6 kwa kuwa aliweza kuwin mipira yote ya juu, dribling safi, kuwepo eneo sahihi kwa muda sahihi na kurudi kusaidia kuchukua mipira katikati.
 
Back
Top Bottom