Viwango vya wanahabari wetu Tanzania viko chini sana

Hizi youtube channel ndo kabisaaa zina wanahabari wa ajabu ajabu siku hizi
Hizo channel ndio zinamilikiwa na wengi wanaojiita graduate wa vyuo vikuu kozi za habarina mawasiliano kwa umma.
 
Nadhani wengi si waandishi bali watu walochungulia fursa au wanapenda fani lakini haWana weledi bado naamini wapo waandishi wazuri ila wanakuwa overshadowed na makanjanja kuna waandishi wazuri sema inawezekana mfumo wa sasa wanajikuta wameaachwa nje ya mfumo mpya wa digitali. Wengi wanashindana kuwa wa kwanza kutoa habari mwandishi lazima awe ni mtu mwemye maarifa na kitu anachokifanya ila wengi waliopo sasa na unaowaona ni wale wenye vichannel you tube na blogs tusiwahukumu kwa ujumla wao.
 
Mkuu Tanzania ukijua kuchekesha tu wewe ni mwanahabari unakabidhiwa kipindi kutangaza.
 
Ndugu mimi nimekuwa nikihoji elimu ya uandishi wa habari kwa hawa waandishi wa habari wa hapa kwetu wanaipata wapi? Au ni wahariri? Yaani utaangalia habari za Tanzania kama huna kifurushi cha televisheni za nje, tunashindwa hata na jirani zetu Uganda na kenya. Cha ajabu haohao wakienda BBC,DW wanatangaza tofauti na wanavyofanya hapa nyumbani. Nawashauri waandishi wa hapa kwetu muwe mnaangalia vyombo vya nje wanavyotangaza mnalinganisha na mnavyofanya hapa, kama hamuoni tofauti au mkiona ninyi ni bora muombe jirani zenu waje wawasaidie kuwaonesha tofauti ilipo na kuwaeleza yapi ni matangazo bora. Kwa kifupi Watanzania wengi sasa hivi hawaangalii vyombo vya hapa nchini kwa udhaifu wanaouonesha
 
Mtangazaji mmoja wa michezo alikuwa anaongelea habari kuhusu Drogba kutaka kuomba ridhaa ya kuliongoza shirikisho la mpira la ivory coast baada ya uongozi wa sasa wa shirikisho hilo kumaliza muda wake. Lakini mtangazaji wakati wa kudadavua kama wa ivory coast watampa Didie Drogba au la mtangazaji huyo akasema wanaweza kumpa Drogba kama sample size ili waone kama mtu wa mpira kama Drogba anaweza kuleta mabadiliko chanya kwenye mpira nchini humo.

Hebu ona namna neno "sample size" lilivyotumika hapa kwenye chombo kinachosikilizwa na dunia nzima. Tungemetemea mwandishi angetumia neno "pilot study" au "Guinea pig" badala ya sample size. Waandishi wetu wanatutia aibu Sisi jamanii
 
hawa waandishi kazi ni kuandika majungu na umbeya wanaweza kumwandama mchezaji wakidai kiwango kimeshuka au kocha hana uwezo sijui wakifukuzwa wanazani hizo pesa zitaenda kwao
 
uko sahihi sana na hasa hawa CLOUDS FM na watangazaji wao Shafi dauda,Edgar Kibwana,Luambano,Issa Maeda ni very poor and hopeless katika hiyo kazi!
Afu kwenye kipindi chao Wana mtu anaitwa Mbwige,sijui role yake huwa ni Nini kwenye kile kipindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…