Viwanja hivi vipanuliwe

Viwanja hivi vipanuliwe

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Kutokana na na hadhi ya majina yake, nashauri viwanja hivi vipanuliwe na viboreshwe keundana inayoendana na hadhi majina yake:

(1) Uwanja wa Karume - Dar
(2) Uwanja wa Sokoine - Mbeya
(3) Uwanja wa Nelson Mandela - Sumbawanga
(4) Uwanja wa Kawawa - Kigoma
(5) Uwanja wa Ali hassan mwinyi - Tabora
(6) Uwanja wa Kambarage - Shinyanga
(7) Uwanja wa Karume - Musoma

Ili kufanikisha azima hii, inabidi Serikali kuu, TFF, na serikali za Mitaa kushirikiana.Serikali kuu igharimie asilimia 35%, jukumu hilo ligawanye kwenye wizara za utalii (kitengo cha kumbukumbu ya mambo ya kale), michezo na wizara inayohusika na Ujenzi. TFF nayo igarimie asilimia 35%, wakati serikali za mitaa kwenye miji ilimo viwanja hivyo igharimie 30% .
 
Umeonyesha kukerwa sana na viwanja hivi kama wanavyokerwa wapenzi wengi soka hapa nchini.. lkn nikuulize kabla hujafikiria kutoa ushauri huu je unawajua wamiliki wa hivyo viwanja?? Hivyo sio viwanja vya serikari wala raia wa Tanzania ingawa wao ndio waliovijenga..

wanaomiliki viwanja hivi wala hawana hata chembe ya kufanya matengenezo. wao vikiwa vibaya kama unavyoviona ndo furaha kwao.... na wala hawapendi kabisa kuona serikari inajenga viwanja vipya na ikitokea kuna bajeti hiyo wanafutilia mbali kabisa ili tuendelee kutumia viwanja vya vibovu.. ukiona kuna uwanja wa serikakari kama ule wa mkapa ujue ni maono ya raisi tu na sio wabunge wala mawaziri wa ccm ..wakikaa bungeni hawajawahi kuongelea masuala ya kujenga viwanja kwa kuhofia kutelekezwa kwa viwanja vyao.
 
Umeonyesha kukerwa sana na viwanja hivi kama wanavyokerwa wapenzi wengi soka hapa nchini.. lkn nikuulize kabla hujafikiria kutoa ushauri huu je unawajua wamiliki wa hivyo viwanja?? Hivyo sio viwanja vya serikari wala raia wa Tanzania ingawa wao ndio waliovijenga.. wanaomiliki viwanja hivi wala hawana hata chembe ya kufanya matengenezo. wao vikiwa vibaya kama unavyoviona ndo furaha kwao.... na wala hawapendi kabisa kuona serikari inajenga viwanja vipya na ikitokea kuna bajeti hiyo wanafutilia mbali kabisa ili tuendelee kutumia viwanja vya vibovu.. ukiona kuna uwanja wa serikakari kama ule wa mkapa ujue ni maono ya raisi tu na sio wabunge wala mawaziri wa ccm ..wakikaa bungeni hawajawahi kuongelea masuala ya kujenga viwanja kwa kuhofia kutelekezwa kwa viwanja vyao.
Nadhani unasema kuwa ni vya CCM, lakini hilo ni jambo ambalo tumewahi kuliongelea hapa huko nyuma kuwa viwanja vyote vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi wakati wa Chama kimoja vinatakiwa virudishwe serikalini. Kwa mfano mimi binafsi nilishiriki ujenzi wa Uwanja wa Kirumba-Mwanza mwaka 1980 na uwanja wa Karume-Musoma miaka ya sabini kama raia wa kawaid tulikuwa tunaenda kusoma matofari na mchanga wakti wa ujenzi; lakini mimi leo siyo mwana CCM. Itakuwaje nguvyu yangu imilikiwe na chama cha siasa ilihali nilijitolea nikijua ni uwanja wa umma?
 
Back
Top Bottom