Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Kama kuna jambo linalokera sana ni pale viwanja vilivyokuwa vya umma kabla ya mfumo wa vyama vingi kuporwa na CCM ambayo imeshindwa kuviendeleza. Inaonekana kama wangekuwa na uwezo walitaka hata jengo la Ikulu liwe la CCM.
Natoa hoja kuwa viwanja vyote ambavyo vilikuwa vya umma kabla ya mfumo wa vyama vingi virudiswhe serikalini kama ilivyo uwanja wa Uhuru.
Mkwakwani, Amri Abeid, Kirumba, Ali Hassan Mwinyi, Nelson Mandela, Samora na vingine vingi virudishwe serikali mara moja; havikujengwa na CCM bali vilijengwa na wananchi wote. Uwanja wa Mkwakwani umekuwapo tangu wakati wa Ukoloni; uwanja wa Amri Abeid ulijengwa kabla hata CCM haijazaliwa; na hata vile vilivyojengwa baada ya CCM havikuwa vimejengwa kama vitega uchumi vya CCM bali vilijengwa kama viwanja vya burudani kwa wanachi wote.
Sijui kama nimeeleweka.