Viwanja Vyote vya Michezo Vipo Tayari Kutumika na CHAN Ifikapo Agosti, 2025

Viwanja Vyote vya Michezo Vipo Tayari Kutumika na CHAN Ifikapo Agosti, 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa maandalizi ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) yanaendelea kwa kasi, huku viwanja vyote vilivyopangwa kwa ajili ya mashindano hayo vikiwa tayari kwa matumizi hata kama michuano ingeanza mwezi ujao.

Kauli hiyo ametoa Mei 30, 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga, aliyeomba kuhakikishiwa kama Tanzania ipo tayari kwa CHAN inayotarajiwa kufanyika Agosti 2025.

Viwanja hivyo ambavyo Mhe Mwinjuma amesema vimekamilika ukarabati wake ni Benjamin Mkapa Dar es salaam, Amaan Zanzibar na viwanja vya mazoezi ambapo Dar es salaam kuna viwanja vitatu kikiwemo kiwanja cha Shule ya Sheria, Gymkana na Meja Jenerali Isamuhyo ambavyo vyote vipo katika hali nzuri.

Screenshot 2025-05-31 at 18-45-58 millardayo • Instagram photos and videos.png
Screenshots_2021-07-06-10-49-34.png
 
Back
Top Bottom