Vizazi vijavyo vikikuta rasilimali si zao vitaanzisha uasi na kuingia msituni kuipinga serikali

chotera

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
6,560
Reaction score
15,864
Angalizo.

Wajukuu na watoto wetu baadae wakija kupata akili wakaona rasilimali za ardhi yao kama bandari si yao tena, ardhi si yao tena, mbuga za wanyama hawana umili nazo tena lazima moto uwake.

Katika kila uwekezaji lazima tuzingatie 50/50 yaani wakija kukuta wana asilimia 50 ya umiliki hapo wataona fahari kwani maana halisi ya kuzaliwa nchini itakuepo.

Lakini wakikuta hawamiliki chochote na wamesoma, nawahakikishieni hawatoishia mitandaoni kwani kila stage unayoiona leo itakua imepita tayari.

Wao wata ingia msituni na kupanga uasi dhidi ya serikali dhalimu na hawatoona mwekezaji kama dhalimu wataona serikali ndio dhalimu kwa kuingia mikataba mibovu na hapo wataanza kwa kuwaumiza wawekezaji, viongozi direct, na hapo itakua too late.

Ili isijekutokea tujitahidi tujadili mambo haya kwa weledi mkubwa kwani impact yake baadae 100 ambayo tutakua hatupo itakua mbaya sana.

Kiongozi ambae leo yupo bungeni, au serikalini 100 miaka hiyo hatokuepo mjue hivo anatakiwa aandae future njema ya wajukuu zake wasigeuke watumwa na waasi.
 
Hili la DP litaingiza watu msituni naona linaanza kuwapa watu ushujaa/ujasiri. Lakini naanza kujhiuliza, hata Jeshi letu halioni uhanithi huu? Litauwa watu wake kutetea nchi yao kuuzwa? sidhani, yaliyo moyoni mwao anajua Mungu
 
Hakuna mtanzania wa hivyo. Acha kuwapa sifa zisizo zao. Yaana kizazi cha access na smartphone na mitandao ya kijamii eti kiingie msituni.

Vijana wenzenu wanne juzi wamejitokeza kuandamana, wakati waliojitokeza kushuhudia na kupiga picha za hao waandamanaji walikua zaidi ya 200 na magari mawili ya Polisi wenye silaha za kivita.
 
Hili la DP litaingiza watu msituni naona linaanza kuwapa watu ushujaa/ujasiri. Lakini naanza kujhiuliza, hata Jeshi letu halioni uhanithi huu ? Litauwa watu wake kutetea nchi yao kuuzwa? sidhani, yaliyo moyoni mwao anajua Mungu

La bandari limeleta mgawanyiko mkubwa kwanza kwa raia mmoja mmoja, lakini limegusa angle za kikanda na kidini ni hatari sana sasa impact yake baadae ndio watu kufanya uasi na kuua wale wanaodhani ni chanzo cha wao kukosa umiliki wa rasilimali zao
 
Hakuna mtanzania wa hivyo. Acha kuwapa sifa zisizo zao. Yaana kizazi cha access na smartphone na mitandao ya kijamii eti kiingie msituni.
Vijana wenzenu wanne juzi wamejitokeza kuandamana, wakati waliojitokeza kushuhudia na kupiga picha za hao waandamanaji walikua zaidi ya 200 na magari mawili ya Polisi wenye silaha za kivita.

Hapo unaleta mzaha ambao sio mzuri tuwakumbushe viongozi wetu wafanye maamuzi mazuri kwa ajili ya leo na kesho njema
 
La bandari limeleta mgawanyiko mkubwa kwanza kwa raia mmoja mmoja, lakini limegusa angle za kikanda na kidini ni hatari sana sasa impact yake baadae ndio watu kufanya uasi na kuua wale wanaodhani ni chanzo cha wao kukosa umiliki wa rasilimali zao
Hili linakuja. Mbowe ametahadhalisha kuwa Samia aangalie watu wasijenge wazo kuwa huyu Kauza Tanganyika ambayo siyo kwao kwa asili, kaacha Zanzibar kwao. Wengi na mimi included nina wazo hilo hata kama Mbowe asingeli hint on that!
 
Mbowe alitoa tahadhari ya kujenga sana lakini wakageuza maneno kisiasa wakaanza kuongea wanayoyajua yao, na hoja ya mbowe ilikua wazi kabisa kuepusha chuki za upande mmoja wa muungano kwenda upande mwingine lakini walivokurupuka kumjibu kama wachawi walikutwa na mwanga wa asubuhi wakiwa wanawanga
 
La bandari limeleta mgawanyiko mkubwa kwanza kwa raia mmoja mmoja, lakini limegusa angle za kikanda na kidini ni hatari sana sasa impact yake baadae ndio watu kufanya uasi na kuua wale wanaodhani ni chanzo cha wao kukosa umiliki wa rasilimali zao
Hi inakuja tena si mbali
 
Hakuna Watanzania waatakaoweza kufanya jambo la kipumbavu na la kipuuzi kama hilo kutokana na sababu kuu nne.

Moja ni hulka na haiba ya Watanzania ambapo kwa kiasi kikubwa sisi ni watu ambao hatupendi sana mikwaruzano na ni watu wapenda amani. Kabla ya uhuru na hata baada ya uhuru hatukuwa ni watu wagomvi, washari ama wapenda vita. Ustaarabu ulitufikia mapema sana.

Mbili ni maendeleo ya elimu na utamdawazi, ambapo kwa kiasi kikubwa kadri siku zinavyoenda ndivyo watu huzidi kupanuka maarifa. Watu wasomi hawapingi mambo kwa kuingia msituni na kufanya uasi bali hutumia njia rafiki katika kujenga hoja za kuipinga serikali, lakini pia kumbuka ya kwamba nchi yetu ina tengeneza mfumo wa watu kuwa wenye kujikomba na kuabudu mamlaka (Uchawa) ili kupata angalau teuzi kidogo maisha yawanyookee.

La Tatu ni uwepo wa intelijensia kali katika kudhibiti mchakato huo, kama taifa tumeshashuhudia chokochoko za majaribu ya mapinduzi mara nyingi ndani ya nchi yetu. Tuliweza vyema kupambana na kadhia hiyo na kuyazima mapinduzi hayo ambayo yalitaka kutokea. Pia kumbuka wale majambazi waliokiwa wakijificha mapangoni kule Amboni na kadhia ya ujambazi kule Kibiti. Matukio yote yanaonyesha uimara wetu katika kudili na aina mbalimbali za matukio.

La Mwisho na hili ndio la msingi, nchi yetu haiuzwi lakini tunafanya mageuzi makubwa baada ya kufeli awali.
Iko hivi, wakati wa awamu ya kwanza, umiliki wa nyanja kuu za uchumi ulidhibitiwa na serikali (sera ya ujamaa na kujitegemea). Katika wakati huu Serikali iliweza kufanya biashara na kuongoza nchi. Sote tunafahamu ni kwa namna gani sera zile zilivyotufukarisha na kukosa huduma za msingi. Waliofuatia walianza utaratibu maalum wa kuanza mchakato wa kubinafsisha nyanja kuu za kiuchumi na zile za msingi zikibaki kwa serikali kwani ilishathibitika ya kuwa mfumo wa kijamaa kamwe hauwezi kufanya kazi nchini na ulishafeli, ukweli ni kwamba kadri siku zilivyokuwa zinasogea basi ndivyo maisha taratibu yanazidi kuimarika kuliko ilivyokuwa awali. Dunia ya sasa ni uwekezaji na kama ni hivyo tunatakiwa tufahamu ni jinsi gani nchi nyingi duniani zilizofungua fursa za uwekezaji leo ni matajiri. Inawezekana kuna makosa kadhaa yapo lakini yanatakiwa yarekebishwe ili yalete tija kwa maslahi mapana ya taifa.

Nchi hii haiuzwi bali inafanyiwa uwekezaji.
 
Unazungumzia intelijensia ipi!.
Watu wanafanya wizi wa mali za umma na ni watanzania wenzetu lakini hawashughulikiwi, mtu mmoja anajiita Kigogo 2014 anetamba bila kukamatwa,n.k.
Sijui umeandika intelijensia ya aina gani, au hujui maana yake.
 
Screenshot_20230622_091504_WhatsApp.jpg
 
Angalizo.

Wajukuu na watoto wetu baadae wakija kupata akili wakaona rasilimali za ardhi yao kama bandari si yao tena, ardhi si yao tena, mbuga za wanyama hawana umili nazo tena lazima moto uwake.

Katika kila uwekezaji lazima tuzingatie 50/50 yaani wakija kukuta wana asilimia 50 ya umiliki hapo wataona fahari kwani maana halisi ya kuzaliwa nchini itakuepo.

Lakini wakikuta hawamiliki chochote na wamesoma, nawahakikishieni hawatoishia mitandaoni kwani kila stage unayoiona leo itakua imepita tayari.

Wao wata ingia msituni na kupanga uasi dhidi ya serikali dhalimu na hawatoona mwekezaji kama dhalimu wataona serikali ndio dhalimu kwa kuingia mikataba mibovu na hapo wataanza kwa kuwaumiza wawekezaji, viongozi direct, na hapo itakua too late.

Ili isijekutokea tujitahidi tujadili mambo haya kwa weledi mkubwa kwani impact yake baadae 100 ambayo tutakua hatupo itakua mbaya sana.

Kiongozi ambae leo yupo bungeni, au serikalini 100 miaka hiyo hatokuepo mjue hivo anatakiwa aandae future njema ya wajukuu zake wasigeuke watumwa na waasi.
Huoni ndichokinachotafutwa na hayo mataifa? Our national security is at stake somebody needs to see this!
 
Angalizo.

Wajukuu na watoto wetu baadae wakija kupata akili wakaona rasilimali za ardhi yao kama bandari si yao tena, ardhi si yao tena, mbuga za wanyama hawana umili nazo tena lazima moto uwake.

Katika kila uwekezaji lazima tuzingatie 50/50 yaani wakija kukuta wana asilimia 50 ya umiliki hapo wataona fahari kwani maana halisi ya kuzaliwa nchini itakuepo.

Lakini wakikuta hawamiliki chochote na wamesoma, nawahakikishieni hawatoishia mitandaoni kwani kila stage unayoiona leo itakua imepita tayari.

Wao wata ingia msituni na kupanga uasi dhidi ya serikali dhalimu na hawatoona mwekezaji kama dhalimu wataona serikali ndio dhalimu kwa kuingia mikataba mibovu na hapo wataanza kwa kuwaumiza wawekezaji, viongozi direct, na hapo itakua too late.

Ili isijekutokea tujitahidi tujadili mambo haya kwa weledi mkubwa kwani impact yake baadae 100 ambayo tutakua hatupo itakua mbaya sana.

Kiongozi ambae leo yupo bungeni, au serikalini 100 miaka hiyo hatokuepo mjue hivo anatakiwa aandae future njema ya wajukuu zake wasigeuke watumwa na waasi.
Mpaka sasa mmefaidika vipi na hizo rasilimali kuwa mikononi mwenu?
 
Hili linakuja. Mbowe ametahadhalisha kuwa Samia aangalie watu wasijenge wazo kuwa huyu Kauza Tanganyika ambayo siyo kwao kwa asili, kaacha Zanzibar kwao. Wengi na mimi included nina wazo hilo hata kama Mbowe asingeli hint on that!
Yaan mimi nasikia uchungu sana na kwakweli kama mtanganyika nawaza sana why wauze bandari???itafika siku ya ukombozi na haiko mbali
 
Huyu maza ake nani? Antafuta lawama
Auza bandari, mwambieni bwana!
 
Hapo unaleta mzaha ambao sio mzuri tuwakumbushe viongozi wetu wafanye maamuzi mazuri kwa ajili ya leo na kesho njema
Mkifanya mzaha na rasilimali za nchi utafika wakati na sio mbali watu wataamua kugawana fito!!! Samia anaturudisha enzi za utumwa wa waarabu wakati ambao Watu walianza kusahau machungu waliopitia babu zao!!
Samia na genge lake wana nyumba DUBAI hivyo wana mahala pa kukimbilia , je sisi makabwela tutakimbilia wapi? LAZIMA PATACHIMBIKA!
 
Back
Top Bottom