Vizazi vijavyo vikikuta rasilimali si zao vitaanzisha uasi na kuingia msituni kuipinga serikali

Vizazi vijavyo vikikuta rasilimali si zao vitaanzisha uasi na kuingia msituni kuipinga serikali

NISIVYO MPENDA MTAWALA WA DUBAI NA GENGE LAKE, NYIE ACHANE TU.
 
Misitu nayo watakuta ishauzwa. Labda kpindi icho kutakuwa na misitu ya online. Watatumiana Link
Na hata ikiwepo hakuna kijana atakaeingia msituni ikiwa vijana wenyewe ndio hawa watoto wa sasa ambao hawawezi kula mpaka waangalie Cocomelon.
Vijana wa kiume wanaojimithilisha na dada zao kimavazi mpaka vitendo.

Vijana wa baadae watarudi rasmi katika ukoloni na kuwa watumwa. Watakuwa watumwa wa kisasa walioshikwa akili, maarifa mpaka maamuzi.

Wakuikomboa hii nchi ilipaswa iwe sisi lakini na sisi tushajitolea kuwa keyboard warriors. Maneno mengi mtandaoni ila tukisikia kuna panya road tunajificha chini ya uvungu wa kitanda.
 
Angalizo.

Wajukuu na watoto wetu baadae wakija kupata akili wakaona rasilimali za ardhi yao kama bandari si yao tena, ardhi si yao tena, mbuga za wanyama hawana umili nazo tena lazima moto uwake.

Katika kila uwekezaji lazima tuzingatie 50/50 yaani wakija kukuta wana asilimia 50 ya umiliki hapo wataona fahari kwani maana halisi ya kuzaliwa nchini itakuepo.

Lakini wakikuta hawamiliki chochote na wamesoma, nawahakikishieni hawatoishia mitandaoni kwani kila stage unayoiona leo itakua imepita tayari.

Wao wata ingia msituni na kupanga uasi dhidi ya serikali dhalimu na hawatoona mwekezaji kama dhalimu wataona serikali ndio dhalimu kwa kuingia mikataba mibovu na hapo wataanza kwa kuwaumiza wawekezaji, viongozi direct, na hapo itakua too late.

Ili isijekutokea tujitahidi tujadili mambo haya kwa weledi mkubwa kwani impact yake baadae 100 ambayo tutakua hatupo itakua mbaya sana.

Kiongozi ambae leo yupo bungeni, au serikalini 100 miaka hiyo hatokuepo mjue hivo anatakiwa aandae future njema ya wajukuu zake wasigeuke watumwa na waasi.
Wacha waliopo WAUZE RASLIMALI ZOTE Wapige Mapesa inawezekana Wataenda nazo MBINGUNI
 
Hakuna Watanzania waatakaoweza kufanya jambo la kipumbavu na la kipuuzi kama hilo kutokana na sababu kuu nne.

Moja ni hulka na haiba ya Watanzania ambapo kwa kiasi kikubwa sisi ni watu ambao hatupendi sana mikwaruzano na ni watu wapenda amani. Kabla ya uhuru na hata baada ya uhuru hatukuwa ni watu wagomvi, washari ama wapenda vita. Ustaarabu ulitufikia mapema sana.

Mbili ni maendeleo ya elimu na utamdawazi, ambapo kwa kiasi kikubwa kadri siku zinavyoenda ndivyo watu huzidi kupanuka maarifa. Watu wasomi hawapingi mambo kwa kuingia msituni na kufanya uasi bali hutumia njia rafiki katika kujenga hoja za kuipinga serikali, lakini pia kumbuka ya kwamba nchi yetu ina tengeneza mfumo wa watu kuwa wenye kujikomba na kuabudu mamlaka (Uchawa) ili kupata angalau teuzi kidogo maisha yawanyookee.

La Tatu ni uwepo wa intelijensia kali katika kudhibiti mchakato huo, kama taifa tumeshashuhudia chokochoko za majaribu ya mapinduzi mara nyingi ndani ya nchi yetu. Tuliweza vyema kupambana na kadhia hiyo na kuyazima mapinduzi hayo ambayo yalitaka kutokea. Pia kumbuka wale majambazi waliokiwa wakijificha mapangoni kule Amboni na kadhia ya ujambazi kule Kibiti. Matukio yote yanaonyesha uimara wetu katika kudili na aina mbalimbali za matukio.

La Mwisho na hili ndio la msingi, nchi yetu haiuzwi lakini tunafanya mageuzi makubwa baada ya kufeli awali.
Iko hivi, wakati wa awamu ya kwanza, umiliki wa nyanja kuu za uchumi ulidhibitiwa na serikali (sera ya ujamaa na kujitegemea). Katika wakati huu Serikali iliweza kufanya biashara na kuongoza nchi. Sote tunafahamu ni kwa namna gani sera zile zilivyotufukarisha na kukosa huduma za msingi. Waliofuatia walianza utaratibu maalum wa kuanza mchakato wa kubinafsisha nyanja kuu za kiuchumi na zile za msingi zikibaki kwa serikali kwani ilishathibitika ya kuwa mfumo wa kijamaa kamwe hauwezi kufanya kazi nchini na ulishafeli, ukweli ni kwamba kadri siku zilivyokuwa zinasogea basi ndivyo maisha taratibu yanazidi kuimarika kuliko ilivyokuwa awali. Dunia ya sasa ni uwekezaji na kama ni hivyo tunatakiwa tufahamu ni jinsi gani nchi nyingi duniani zilizofungua fursa za uwekezaji leo ni matajiri. Inawezekana kuna makosa kadhaa yapo lakini yanatakiwa yarekebishwe ili yalete tija kwa maslahi mapana ya taifa.

Nchi hii haiuzwi bali inafanyiwa uwekezaji.
Nonsense.

"Nchi haiuzwi lakini mnafanya mageuzi makubwa"

Hayo mageuzi makubwa ya kuwamilikisha wageni rasilimali zetu milele yana maana gani kwa vizazi vijavyo?

Taifa halina kiongozi, watanganyika tuna hasara sana.
 
Yaani washindwe vijana wa Sasa wanaoona hizo Mali zao zikiuzwa waje waingie msituni vijana ambao watasimuliwa na babu zao[emoji848]?

Mwandishi haupo serious.
 
Back
Top Bottom