Vladimir Putin asema Urusi ina kombora 'lisiloweza kuzuiwa' na Marekani

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Urusi inamiliki kombora ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin.
Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale.
Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo.
Huku akitumia skrini kubwa, alionyesha video za alichosema ni kombora jipya la Urusi.
Alisema kombora hilo haliwezi kuzuiwa na mfumo wa kinga wa makombora wa Marekani barani Ulaya na Asia.
Kadhalika, ameonesha video ya ndege isiyo na rubani inayoweza kufanya kazi chini ya bahari.
Kwenye hotuba hiyo yake kwa kikao cha pamoja cha mabunge mawili, aliwahamasisha raia kupendekeza majina ya kupewa mifumo hiyo miwili ya silaha

Ulinzi​

Putin alisema uwezo wa kijeshi wa Urusi umepangwa na kustawishwa kwa lengo la kudumisha amani duniani.
Hata hivyo, amesema iwapo mtu yeyote yule atathubutu kurusha silaha za nyuklia dhidi ya Urusi, atajibiwa mara moja.
Operesheni ya kijeshi ya Urusi Syria, ambapo anasaidia Rais wa Syria Bashar al-Assad dhidi ya waasi na amesema hiyo inadhihirisha kuimarika kwa uwezo wa Urusi katika kujilinda.
Urusi iliteka Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 wakati wa uongozi wa Bw Putin.
Kiongozi huyo amesema Urusi inalinda maslahi yake katika eneo la Arctic kwa kuimarisha miundo mbinu yake ya kijeshi eneo hilo.
 
Hii habari ya miaka mingi namna hii wewe ndio inafika kwako?😄
 
Putin na tabia za paka kujivimbisha aonekane mkubwa....na hawezi acha hii tabia. Kuanzisha vita nyingine wakati Kila siraha umetumia Ukraine
 
Putin kachanganyikiwa. Maneno mengi, uhalisia tofauti.

Alisema ataiteka Kiev, na kuiondoa Serikali ya Ukraine, ndani ya siku mbili. Leo ni miaka. Huyu ni wa kupuuzwa.
 
Assad kumbe bado rais wa Syria au Putin bado yuko mwaka 2012 na anaendelea kumlinda?
 
Urusi inamiliki kombora ambalo haliwezi kutunguliwa na linaweza kufika pahala popote duniani, kwa mujibu wa Rais Vladimir Putin.
Amesema kombora "halipai juu sana, ni vigumu sana kulitambua likipita, lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia na linaweza kufika popote pale.
Aidha, njia linayofuata haiwezi kutabirika na adui, linaweza kukwepa vizuizi na kimsingi haliwezi kuzuiwa na mifumo ya sasa ya kinga dhidi ya makombora na hata mifumo inayotarajiwa kuundwa siku zijazo.
Huku akitumia skrini kubwa, alionyesha video za alichosema ni kombora jipya la Urusi.
Alisema kombora hilo haliwezi kuzuiwa na mfumo wa kinga wa makombora wa Marekani barani Ulaya na Asia.
Kadhalika, ameonesha video ya ndege isiyo na rubani inayoweza kufanya kazi chini ya bahari.
Kwenye hotuba hiyo yake kwa kikao cha pamoja cha mabunge mawili, aliwahamasisha raia kupendekeza majina ya kupewa mifumo hiyo miwili ya silaha

Ulinzi​

Putin alisema uwezo wa kijeshi wa Urusi umepangwa na kustawishwa kwa lengo la kudumisha amani duniani.
Hata hivyo, amesema iwapo mtu yeyote yule atathubutu kurusha silaha za nyuklia dhidi ya Urusi, atajibiwa mara moja.
Operesheni ya kijeshi ya Urusi Syria, ambapo anasaidia Rais wa Syria Bashar al-Assad dhidi ya waasi na amesema hiyo inadhihirisha kuimarika kwa uwezo wa Urusi katika kujilinda.
Urusi iliteka Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 wakati wa uongozi wa Bw Putin.
Kiongozi huyo amesema Urusi inalinda maslahi yake katika eneo la Arctic kwa kuimarisha miundo mbinu yake ya kijeshi eneo hilo.
Nina uhakika ungeomba kuteuliwa kugombea Ubunge CCM jina lako lisingerudi. Chama na serikali kinataka maendeleo na sio mtu anayeturudisha nyuma
 
Back
Top Bottom