Vladimir Putin ataka mateka wa Kirusi kuishukuru Hamas kwa kuwaachia huru

Vladimir Putin ataka mateka wa Kirusi kuishukuru Hamas kwa kuwaachia huru

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
9,662
Reaction score
8,023
Wakuu,

Vladimir Putin alikutana na Sasha Troufanov, mateka wa Kirusi-Mwizraeli aliyeachiliwa baada ya kushikiliwa kwa karibu siku 500 huko Gaza, na kumhimiza amshukuru mtekaji wake wa Hamas kwa “kitendo cha kibinadamu” cha kumuachilia.

“Ukweli kwamba uliweza kuachiwa ni matokeo ya kuwa Urusi ina mahusiano ya kudumu na thabiti na watu wa Palestina, na wawakilishi wao, pamoja na mashirika mbalimbali,” alisema rais huyo wa Urusi kwa Troufanov katika Ikulu ya Kremlin, ambapo aliambatana na mama yake, Elena Trufanova, na mpenzi wake, Sapir Cohen, ambao pia walitekwa na Hamas.

“Nadhani tunapaswa kutoa maneno ya shukrani kwa upande wa kisiasa wa Hamas kwa kushirikiana nasi na kutekeleza kitendo hiki cha kibinadamu,” alisema Putin katika kipande cha video kilichowekwa na kituo cha habari kinachofadhiliwa na serikali ya Urusi, RT.

Putin aliongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Hamas kuhakikisha mateka wengine wanaachiliwa, na alitikisa kichwa kwa mshangao baada ya Troufanov kumwambia kuwa alishikiliwa kwa siku 498, kwa mujibu wa video hiyo.

 
Mkuu kwani ni nchi zote duniani zimeitambua Hamas kama kundi la magaidi? Ila pia sidhani kama unaweza kuwa na akili unayodai anayo Putin ukaweza kuongoza taifa namba 2 duniani kwa nguvu za kijeshi.
 
Mkuu hujui diplomasia na kaa kimya. Je mateka wameisha? Wangeweza kuwaua wote pia, mungefanya Nini, lakini kuwaacha hai na kuwatunza hadi walipokabidhiwa kulikua na haja ya kushukuru. Lakini pia Kuna wanaoshikiliwa Bado hivyo Kuna haja ya kushukuru ndio diplomasia. Kumbuka Rais ndio mwanadiplomasia mkuu wa nchi
 
Katika mkutano wa Kremlin na mateka walioachiliwa Sasha Troufanov, mama yake Elena, na mshirika Sapir Cohen, Rais wa Urusi Vladimir Putin alikiri kuachiliwa kwao kwa uhusiano wa Urusi na Hamas na akatoa "shukrani" kwa viongozi wa kisiasa wa kundi la kigaidi-licha ya Hamas kumuua babake Troufanov mnamo Oct 7,2023.

Hii inashangaza sana kwa Mkuu wa nchi kuwashukuru Magaidi wa Hamas ambao waliamua baba yake harafu wanapewa shukrani na Mkuu wa nchi Putin wakati kuachiliwa kwao Israel ilibidi iwaachie mamia ya magaidi ambao walikuwa Wame fungal huko Israel kwa makosa ya Ugaidi na mauaji ya watu wasio na hatia.

Putin alisema Urusi itaendelea kufanya kazi ili kupata matokeo zaidi na akapongeza Hamas kwa ushirikiano. Mkutano huo ulijumuisha viongozi wa Kiyahudi wa Urusi na kuangazia uratibu unaoendelea wa Moscow na washiriki wote katika Mashariki ya Kati, pamoja na Hamas, ambayo ilishatangazwa kama shirika la kigaidi na Amerika, EU, na Israeli.
Akili za Echolima1: zimechanganyikana na makamasi pia. Pumbafffff Echolima1:
 
Who is the top powerful leader in the world?
Gallery of top ten in rankings 2018
  • Xi Jinping.
  • Vladimir Putin.
  • Donald Trump.
 
Putin lazima awashangae Hamas,,,,yeye wale Mateka wake WA Ukraine,anachofanya ni kuwavua magwanda ya Ukraine na kuwavesha ya urusi,anawapatia Ak 47,anawapa semina ya dk kadhaa chini ya mti,anawageuza walikotokea wananaichapa nchi Yao.
 
Akili za Echolima1: zimechanganyikana na makamasi pia. Pumbafffff Echolima1:
Una bahati jana tu nilikuwa nimetembelea kaburi la Yusuph huko Nablus magaidi wenzako wakawa wanaturushia mawe uzuri walikumbana na mkono wenye nguvu wa majeshi ya Israel. Huyu putin mjinga sana anawaambiaje wawashukuru Hamas kwanza hao hao hamas waliua baba yao hizo akili zake zimejaa Makamasi !!
 

Attachments

  • IMG_9025.mp4
    5.8 MB
Putin aliisha jichafua na kukimbiwa na marafiki kufuatia sera zake za hovyo za kutaka kujitanua na sasa anatafuta tena marafiki hata kama ni magaidi. Putin bure kabisa.
 
Una bahati jana tu nilikuwa nimetembelea kaburi la Yusuph huko Nablus magaidi wenzako wakawa wanaturushia mawe uzuri walikumbana na mkono wenye nguvu wa majeshi ya Israel. Huyu putin mjinga sana anawaambiaje wawashukuru Hamas kwanza hao hao hamas waliua baba yao hizo akili zake zimejaa Makamasi !!
mkuu sijakuona kwenye hii clip
 
Back
Top Bottom