Vladimir Putin ataka mateka wa Kirusi kuishukuru Hamas kwa kuwaachia huru

Echolima1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2019
Posts
9,662
Reaction score
8,023
Wakuu,

Vladimir Putin alikutana na Sasha Troufanov, mateka wa Kirusi-Mwizraeli aliyeachiliwa baada ya kushikiliwa kwa karibu siku 500 huko Gaza, na kumhimiza amshukuru mtekaji wake wa Hamas kwa “kitendo cha kibinadamu” cha kumuachilia.

“Ukweli kwamba uliweza kuachiwa ni matokeo ya kuwa Urusi ina mahusiano ya kudumu na thabiti na watu wa Palestina, na wawakilishi wao, pamoja na mashirika mbalimbali,” alisema rais huyo wa Urusi kwa Troufanov katika Ikulu ya Kremlin, ambapo aliambatana na mama yake, Elena Trufanova, na mpenzi wake, Sapir Cohen, ambao pia walitekwa na Hamas.

“Nadhani tunapaswa kutoa maneno ya shukrani kwa upande wa kisiasa wa Hamas kwa kushirikiana nasi na kutekeleza kitendo hiki cha kibinadamu,” alisema Putin katika kipande cha video kilichowekwa na kituo cha habari kinachofadhiliwa na serikali ya Urusi, RT.

Putin aliongeza kuwa ataendelea kushirikiana na Hamas kuhakikisha mateka wengine wanaachiliwa, na alitikisa kichwa kwa mshangao baada ya Troufanov kumwambia kuwa alishikiliwa kwa siku 498, kwa mujibu wa video hiyo.

Your browser is not able to display this video.
 
Mkuu kwani ni nchi zote duniani zimeitambua Hamas kama kundi la magaidi? Ila pia sidhani kama unaweza kuwa na akili unayodai anayo Putin ukaweza kuongoza taifa namba 2 duniani kwa nguvu za kijeshi.
 
Mkuu hujui diplomasia na kaa kimya. Je mateka wameisha? Wangeweza kuwaua wote pia, mungefanya Nini, lakini kuwaacha hai na kuwatunza hadi walipokabidhiwa kulikua na haja ya kushukuru. Lakini pia Kuna wanaoshikiliwa Bado hivyo Kuna haja ya kushukuru ndio diplomasia. Kumbuka Rais ndio mwanadiplomasia mkuu wa nchi
 
Akili za Echolima1: zimechanganyikana na makamasi pia. Pumbafffff Echolima1:
 
Who is the top powerful leader in the world?
Gallery of top ten in rankings 2018
  • Xi Jinping.
  • Vladimir Putin.
  • Donald Trump.
 
Putin lazima awashangae Hamas,,,,yeye wale Mateka wake WA Ukraine,anachofanya ni kuwavua magwanda ya Ukraine na kuwavesha ya urusi,anawapatia Ak 47,anawapa semina ya dk kadhaa chini ya mti,anawageuza walikotokea wananaichapa nchi Yao.
 
Akili za Echolima1: zimechanganyikana na makamasi pia. Pumbafffff Echolima1:
Una bahati jana tu nilikuwa nimetembelea kaburi la Yusuph huko Nablus magaidi wenzako wakawa wanaturushia mawe uzuri walikumbana na mkono wenye nguvu wa majeshi ya Israel. Huyu putin mjinga sana anawaambiaje wawashukuru Hamas kwanza hao hao hamas waliua baba yao hizo akili zake zimejaa Makamasi !!
 

Attachments

  • IMG_9025.mp4
    5.8 MB
Putin aliisha jichafua na kukimbiwa na marafiki kufuatia sera zake za hovyo za kutaka kujitanua na sasa anatafuta tena marafiki hata kama ni magaidi. Putin bure kabisa.
 
mkuu sijakuona kwenye hii clip
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…