VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Tanzania na Ethiopia zimesaini mikataba kadhaa na Korea Kusini kwa ajili ya kupata mikopo ya mabilioni ya dola kwa ajili ya maendeleo.

Mikopo hiyo itaiwezesha Korea Kusini kupata fursa ya kuchimba madini muhimu katika nchi za Afrika.

Korea Kusini imeandaa kongamano na viongozi 30 wa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania na Ethiopia.

Kongamano linafanyika wiki hii

Tanzaia imesema kwamba itakopa dola bilioni 2.5 kutoka kwa Korea Kusini katika muda wa miaka mitano ijayo. Mkopo huo utalipwa katika muda wa miaka 5.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan vile vile amesaini mkataba utakaoiruhusu Korea Kusini kutumia bahari yake na madini yanayotumika katika teknolojia ya nishati safi kama Nickel, Lithium na Graphite.

Ethiopia nayo imesaini mkopo wa dola bilioni 1 utakaolipwa katika kipindi cha miaka minne kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, sayansi na teknolojia, afya na maendeleo ya mijini.

PIA SOMA
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

- Prof. Kitila Mkumbo akanusha masharti ya Mkopo wa Korea Kusini

Voice of America
Unasoma kila habari juu ya huu mkopo, huoni nibkwa akili ya nini? Ethiopia wameeleza kwa ufasaha, watatumia aje mkopo wao. Sisi tunakopa tu, zisije ishia kwenye benki za wanaokuka kwa urefu wa kamba zao!
 
Mkuu unataka wananchi waitishe mkutano na kufanya maamuzi kuhusu ilo? Viongozi wanatenda kwa niaba ya watanzania
Viongozi wenyewe wanatenda kiupofu kwasababu ya ulafi wao wa mali za umma.
Ten percent zinawapa upofu na kufanya maamuzi kiupofu kiasi kituingiza shimoni.
 
Viongozi wenyewe wanatenda kiupofu kwasababu ya ulafi wao wa mali za umma.
Ten percent zinawapa upofu na kufanya maamuzi kiupofu kiasi kituingiza shimoni.
Hii ni mada mpya lakini.Kusema kua viongozi hao hawana dhamana na wananchi sio sahihi ata kidogo
 
Hii ni mada mpya lakini.Kusema kua viongozi hao hawana dhamana na wananchi sio sahihi ata kidogo
Dhamana inatakiwa iende sambamba na matakwa yenye tija ya wananchi.
Sio kisa umepewa dhamana basi wajiamulia tu kiulafi ulafi.
 
Ruto nae yuko njiani kwenda huko,
Wanapishana tu na kupungiana mikono angani
Kwenda kuomba mikopo
 
Tatizo habari tumeisikia kutoka vyombo vya nje. Serikali inapaswa kuliweka wazi hili ili wananchi waelewe madhumuni makuu ya huo mkopo na uchimbaji wa hayo madini kama sehemu ya uwekezaji wa nchi ya Korea Tanzania au ni sharti la kupata huo mkopo wa matrilioni
Vyombo vya nje ndo vyakuamini sasa unataka tbc wakupe habari amabayo unapenda kuisikia, vyombo vya nje havirembi mwandiko wanatoa habari kavukavu
 
Tanzania na Ethiopia zimesaini mikataba kadhaa na Korea Kusini kwa ajili ya kupata mikopo ya mabilioni ya dola kwa ajili ya maendeleo.

Mikopo hiyo itaiwezesha Korea Kusini kupata fursa ya kuchimba madini muhimu katika nchi za Afrika.

Korea Kusini imeandaa kongamano na viongozi 30 wa nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania na Ethiopia.

Kongamano linafanyika wiki hii

Tanzaia imesema kwamba itakopa dola bilioni 2.5 kutoka kwa Korea Kusini katika muda wa miaka mitano ijayo. Mkopo huo utalipwa katika muda wa miaka 5.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan vile vile amesaini mkataba utakaoiruhusu Korea Kusini kutumia bahari yake na madini yanayotumika katika teknolojia ya nishati safi kama Nickel, Lithium na Graphite.

Ethiopia nayo imesaini mkopo wa dola bilioni 1 utakaolipwa katika kipindi cha miaka minne kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu, sayansi na teknolojia, afya na maendeleo ya mijini.

PIA SOMA
- Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

- Prof. Kitila Mkumbo akanusha masharti ya Mkopo wa Korea Kusini

Voice of America
Huu upuuzi wa VOA niliuona Toka Jana.Ikumbukwe VOA imekuwa inafanya kampeni ya kuicuafua Tanzania sana Toka awamu ya Magufuli.

Sasa Kwa maelezo haya ya Serikali wanaweza kuweka chanzo Cha taarifa walizonukuu zinazoeleza tofauti na maelezo haya ya Serikali? 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C7yRSIQNIhC/?igsh=MXJjanc0a2J5YmN5eg==
 
Ifike mahala hiyo mikataba iwe ni between wao kwa wao na sio wananchi.. mikataba iwe na limit ya uwepo wao madarakani wakiondoka ndio iwe kikomo hapo upuuzi utaisha.
 
Tatizo habari tumeisikia kutoka vyombo vya nje. Serikali inapaswa kuliweka wazi hili ili wananchi waelewe madhumuni makuu ya huo mkopo na uchimbaji wa hayo madini kama sehemu ya uwekezaji wa nchi ya Korea Tanzania au ni sharti la kupata huo mkopo wa matrilioni
Serikali ilishasema mambo ya mikopo ni siri, uwazi gani tena unaouhitaji...ishu ya bandari iliwekwa wazi mkageuka mbogo! kuwa mpole, Watanzania elekezeni mahaba yenu kwa team za simba na yanga, mambo ya rasilimali za nchi sio kipaumbele chenu...
 
Hao watoto wapo Mkuranga kwa sasa wamenyorodoka, mgao wa mauzo ya ghorofa za kurithi ulikata mwaka mmoja tu baada ya kugawiwa.

Hawana kitu kabisa, huwezi amini kama waliwahi rithishwa maghorofa kariakoo.
Hahahahaha oya acha kabisa yani, lile swala la tunataka maendeleo ya watu kwa kuuza vitu huwa nalipinga sana. Tunakoelekea wote tutabakia wakiwa maana maeneo yote tukiwapa wageni tutaanza ugomvi wa ardhi kama Kenya.
 
Tunakuja kutesa vizazi kulipa madeni ambayo yangeepukika,

punguza matumizi ya Serikali, punguza ukubwa wa Serikali na mavyeo yasiyonamaana, punguza mishahara ya wabunge na posho, ondoa safari zisizo na tija za watumishi, Bana kabisa na komesha wizi na rushwa, JIFANYIE ASSESMENT KWA MWAKA UONE KAMA HUJAPATA 1 trilioni.
Nani mwenye dhamira hiyo kwa sasa ukiwatazama nyuso zao?
 
Back
Top Bottom