VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Unasoma kila habari juu ya huu mkopo, huoni nibkwa akili ya nini? Ethiopia wameeleza kwa ufasaha, watatumia aje mkopo wao. Sisi tunakopa tu, zisije ishia kwenye benki za wanaokuka kwa urefu wa kamba zao!
 
Mkuu unataka wananchi waitishe mkutano na kufanya maamuzi kuhusu ilo? Viongozi wanatenda kwa niaba ya watanzania
Viongozi wenyewe wanatenda kiupofu kwasababu ya ulafi wao wa mali za umma.
Ten percent zinawapa upofu na kufanya maamuzi kiupofu kiasi kituingiza shimoni.
 
Viongozi wenyewe wanatenda kiupofu kwasababu ya ulafi wao wa mali za umma.
Ten percent zinawapa upofu na kufanya maamuzi kiupofu kiasi kituingiza shimoni.
Hii ni mada mpya lakini.Kusema kua viongozi hao hawana dhamana na wananchi sio sahihi ata kidogo
 
Hii ni mada mpya lakini.Kusema kua viongozi hao hawana dhamana na wananchi sio sahihi ata kidogo
Dhamana inatakiwa iende sambamba na matakwa yenye tija ya wananchi.
Sio kisa umepewa dhamana basi wajiamulia tu kiulafi ulafi.
 
Ruto nae yuko njiani kwenda huko,
Wanapishana tu na kupungiana mikono angani
Kwenda kuomba mikopo
 
Vyombo vya nje ndo vyakuamini sasa unataka tbc wakupe habari amabayo unapenda kuisikia, vyombo vya nje havirembi mwandiko wanatoa habari kavukavu
 
Huu upuuzi wa VOA niliuona Toka Jana.Ikumbukwe VOA imekuwa inafanya kampeni ya kuicuafua Tanzania sana Toka awamu ya Magufuli.

Sasa Kwa maelezo haya ya Serikali wanaweza kuweka chanzo Cha taarifa walizonukuu zinazoeleza tofauti na maelezo haya ya Serikali? 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C7yRSIQNIhC/?igsh=MXJjanc0a2J5YmN5eg==
 
Ifike mahala hiyo mikataba iwe ni between wao kwa wao na sio wananchi.. mikataba iwe na limit ya uwepo wao madarakani wakiondoka ndio iwe kikomo hapo upuuzi utaisha.
 
Serikali ilishasema mambo ya mikopo ni siri, uwazi gani tena unaouhitaji...ishu ya bandari iliwekwa wazi mkageuka mbogo! kuwa mpole, Watanzania elekezeni mahaba yenu kwa team za simba na yanga, mambo ya rasilimali za nchi sio kipaumbele chenu...
 
Hao watoto wapo Mkuranga kwa sasa wamenyorodoka, mgao wa mauzo ya ghorofa za kurithi ulikata mwaka mmoja tu baada ya kugawiwa.

Hawana kitu kabisa, huwezi amini kama waliwahi rithishwa maghorofa kariakoo.
Hahahahaha oya acha kabisa yani, lile swala la tunataka maendeleo ya watu kwa kuuza vitu huwa nalipinga sana. Tunakoelekea wote tutabakia wakiwa maana maeneo yote tukiwapa wageni tutaanza ugomvi wa ardhi kama Kenya.
 
Nani mwenye dhamira hiyo kwa sasa ukiwatazama nyuso zao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…