BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Wafanyabiashara katika Mji wa Mlowo, Mbozi wamedaiwa kupandisha vocha za mitandao ya simu toka bei halisi na kuongeza kiwango kati ya shilingi 100 hadi 200 kutokana na eneo hali ilioibuka malalamiko kwa watumiaji wa mitandao ya simu.
Wakiongea malalamiko yao mbele ya mwandishi wetu wamedai imekuwa ni kawaida ya wafanyabiashara kupandisha vocha hasa kipindi hiki cha kuelekea katika bajeti.
"Tunaomba serikali iwachukulie hatua na kuwatia hatiani baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waamini mfano vocha ya 500 tunanunua 600 na vocha ya 1000 tunanunua 1200 sasa huku ni kutuumiza jamani" alisema John Milango mkazi wa forest.
Akiongea mmoja wa wafanyabiashara wa vocha ambae aliomba jina lake lihifadhiwe alidao nao wamekumbana na ongezeko la bei toka kwa wafanyabiashara wa jumla wa vocha wamewapandishia bei ya vocha hivyo imepekea nao kupandisha.
Chanzo: habarijamiitanzania
===========
Nimeona hii taarifa nikaamua kushea hapa, ukweli ni kuwa Wananchi wengi tunaumizwa na hiki kitu, TCRA na TCRA CC mkoa wapi raia tunaumizwa.
Dunia ya Digitali bado upatikanaji wa vocha ni changamoto.
Pia soma - Serikali yaiagiza TCRA kufatilia wanaouza vocha tofauti na bei elekezi