DOKEZO Vocha za Mitandao ya simu zadaiwa kupandisha bei kiholela Mbozi

DOKEZO Vocha za Mitandao ya simu zadaiwa kupandisha bei kiholela Mbozi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Naona upepo umebadilika kabisa kwa members kumshambulia mleta mada kwa kua too manual and not auto, then hoja yake ya msingi imemezwa ghafla...teh😂
 
Ukinunua vocha kama hiyo umeamua kujidhulumu mwenyewe,utanunuaje kitu cha thamani fulani ambayo imeandikwa kabisa kwa bei ya juu!
 
Ila umesema nn? [emoji23][emoji23][emoji23]
Narudia nimesema ukijiona unaweka vocha za kukwangua ujue upo kwenye kundi la watu masikini.

Tajiri hana muda wa kukwangua vocha. Na kuingiza namba moja moja za vocha

Alafu umasikini sio dhambi coca......
 
Hii niliikuta Kibosho pia 😅, Vocha imeandikwa 500 jamaa wa duka anauza 600 na ishakuwa kawaida tu kama hutaki inakubidi uchomoke bush hai town sasa utachagua uongeze 100 au upande boda ya 1000 😅
 

Wafanyabiashara katika Mji wa Mlowo, Mbozi wamedaiwa kupandisha vocha za mitandao ya simu toka bei halisi na kuongeza kiwango kati ya shilingi 100 hadi 200 kutokana na eneo hali ilioibuka malalamiko kwa watumiaji wa mitandao ya simu.

Wakiongea malalamiko yao mbele ya mwandishi wetu wamedai imekuwa ni kawaida ya wafanyabiashara kupandisha vocha hasa kipindi hiki cha kuelekea katika bajeti.

"Tunaomba serikali iwachukulie hatua na kuwatia hatiani baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waamini mfano vocha ya 500 tunanunua 600 na vocha ya 1000 tunanunua 1200 sasa huku ni kutuumiza jamani" alisema John Milango mkazi wa forest.

Akiongea mmoja wa wafanyabiashara wa vocha ambae aliomba jina lake lihifadhiwe alidao nao wamekumbana na ongezeko la bei toka kwa wafanyabiashara wa jumla wa vocha wamewapandishia bei ya vocha hivyo imepekea nao kupandisha.

Chanzo: habarijamiitanzania

===========


Nimeona hii taarifa nikaamua kushea hapa, ukweli ni kuwa Wananchi wengi tunaumizwa na hiki kitu, TCRA na TCRA CC mkoa wapi raia tunaumizwa.

Dunia ya Digitali bado upatikanaji wa vocha ni changamoto.
Lazima zipande kwani sasa meli zinapitia South Africa.
 
Back
Top Bottom