vodacom- hao washindi wa mapikipiki na hela mnawatangaza wapi?

vodacom- hao washindi wa mapikipiki na hela mnawatangaza wapi?

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Wadau,
Kila siku nasikia tu shinda pikipiki tano na shs Milioni mbili...binafsi ningetegemea nione majina ya washindi kama tulivyp zoea kuyaona kwenye promosheni nyingine yakiwa waziwazi kwenye TV au pengine radio (asubuhi/jioni) watu wengi wakifuatilia.
Binafsi sijaona wala sijasikia mtu aliyeshinda...au ndio wanatangaza kwenye magazeti yenye nakala laki mbili (yanayo ishia mijini) wakati watanzania wapo Milioni 40?
Vodacom - kazi ni kwako...
 
Mjini Mipango ndugu! Letatutigite mapesa ya wadanganyika hayo mambo ya promotions ni uwongo mtupu hakuna mshindi bali ni usanii tu!!
 
Mh,
Jamani sijui kama ni watazamaji wazuri wa TV.
Mie Binafsi nimeona wametangaza washindi kwenye TV na majina na pia wameonyeshwa wakati wakikadhibiwa.

Wasiwasi wangu ni kwamba unahofu tu ya bahati nasibu hii,we endelea kushiriki ila kama unaona pesa zako nyingi zimeliwa basi unaweza kuacha.
Siku zote bahati nasibu ni kwamba jichangieni wenyewe then mmoja wenu ndio apatae zawadi.
 
nashukuru kwa uchangiaji wako Zanzibar Spices;
Just a point of interest, washindi ni kila siku washindi sita, najua kabla ya shindao kuanza lazima kuna muda maalum wa kutoa matokeo ambao Vodacom wameingia mkataba na vituo vya matangazo (TV/Radio). Naomba unijulishe ni Tv gani na ni saa ngapi wanarusha matokeo....
Nimesikia vijana wengi wanalalamika kuwa matokeo hayatoki/hawayasikii napengine yanayo toka ni machache sana sio washindi sita kwa siku ( watano pikipiki na mmoja shs milioni 2; nikaona nijaribu kufanya utafiti...
 
natamani wasitoe pikipiki hata moja

hivi hiii kero ya bodaboda hamuioni?

zimekuwa nyiiingi mno sasa

i wish ushuru uongezwe zipunguzwe
 
The boss,
shida sio pikipiki, shida ni waendeshaji...
Nikijaribu kuangalia miji ya wenzetu bado pikipiki zetu ni chache;
Fuailia miji ya china zinakotoka uone pikipiki na baiskeli labda mara 5 ya tulizo nazo ila watu wanajua kuzitumia vizuri na kwa utaratibu...
Tofauti ni kuwa kwa wenzetu wanazitumia kama njia mbadala ya kujirahisishia usafiri wa binafsi na sio kwa biashara...
Kuhusu voda...Watu wanasema mtaani kuwa wanachakachua...ila sina hakika ndio sababu nikavutiwa kujaribu kufuatilia...
 
natamani wasitoe pikipiki hata moja

hivi hiii kero ya bodaboda hamuioni?

zimekuwa nyiiingi mno sasa

i wish ushuru uongezwe zipunguzwe

Serikali ya ccm imeondoa kodi kwa pikipiki ili kupata kura za hao waendeshaji hata kama sio zao LAKINI KUMBE ndio WANAPUNGUZA IDADI ya wapiga kura KWA VIFO NA VILEMA wanaotokana na AJALI ZA BODABODA!
 
Wadau,
Kila siku nasikia tu shinda pikipiki tano na shs Milioni mbili...binafsi ningetegemea nione majina ya washindi kama tulivyp zoea kuyaona kwenye promosheni nyingine yakiwa waziwazi kwenye TV au pengine radio (asubuhi/jioni) watu wengi wakifuatilia.
Binafsi sijaona wala sijasikia mtu aliyeshinda...au ndio wanatangaza kwenye magazeti yenye nakala laki mbili (yanayo ishia mijini) wakati watanzania wapo Milioni 40?
Vodacom - kazi ni kwako...

Kweli mitanzania ni mirahisi sana kudanganyika.
Ivi ukitajiwa majini ndo utaamini kuna mshindi?!
Nakutungia majina 100 apa ndani ya dk 1.
97 - Grace Mohamed - Simanjiro.
98 - Mwanaasha John - Simiyu
99 - Mwamvita Swalehe - Biharamulo
100 - Shabani Ally - G/mboto.

Vp! umeamini washindi wanaweza patikana?!
 
Back
Top Bottom