Vodacom hiki mnachokifanya kwa wateja wenu ni uhuni wa hali ya juu sana. Jirekebisheni haraka iwezekanavyo

Dah! Mkuu umenikumbusha miaka imepita, kuna wizi tulifanyiwa watumishi wa Wizara flani bila ya sisi wadau kuhisi ama kugundua kuibiwa, yaani mpaka leo huwa sihisi wala kuamini kama nami ni mmoja wapo kati ya walioporwa!

Kijana wa It makao makuu aliprogram makato ya sh.500 toka katika mishahara ya kila mwezi ya kila mmoja wetu.

Embu fikiria loss ya sh.500 utaigunduaje katika mshahara wako?

Na wizara ilikuwa na watumishi zaidi ya 40000, hapo piga hesabu, jibu utakalolipata, ndiyo hela alikuwa akitia kibindoni mwake kila mwezi!

Kijana akatajirika hadi akavimbewa kwa kufuru.

Sijui pesa za bure huwaga zina laana gani tu, maana life style yake ndiyo iliyofanya watu waanze kujiuliza: "huu utajiri wa kutisha kaupata wapi huyu kinda.

Kwani walimkawiza.
 
Voda naitumia sababu nilipo ndio mtandao pekee unaosababisha niwe mtandaoni bila kusumbuka 4G
Nikiwa mjini tiGO na Halotel
 
Voda ni kwa wateja wenye matumizi ya utopolo na utopolo wenyewe. Voda ni vibaka watupu
 
Mnaosema ni data ime kata sh100 au 200 sio kweli maaana data ina kata haswaaa within seconds una weza kuta sh 0.

Hapo mteja ume unganishwa na vihuduma vyao kama SOKALETU tazama kama huna hizo text kila zikiingia tu wana kata tshs 200 una letewa habari Ligikuu bara hapo mzee wame kuunga makusudi kama wanavo tuunga wateja wengine ili watule masalio yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…