KERO Vodacom huduma kwa wateja ni tatizo

KERO Vodacom huduma kwa wateja ni tatizo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nimepitia comments nyingi hapa inaonekana kuna tatizo hasa kwa wasimamizi wa hii mitandao, TCRA. Watu wanapolalamikia huduma kuwa mbovu, tcra wanatakiwa kujitokeza na kutolea ufafanuzi jinsi wanavyoyashughulikia. Mfano, watu wananunua huduma mbali mbali kupitia mitandao kama vile luku. Inapotokea huduma ya luku haipatikani, wenye mitandao ukifanya mwamala wa luku wanakukata tu pesa yako lakini hupati token! Ukiwauliza wanakwambia tu huduma haipatikani lakini tayari wameshakula pesa yako na hairudi hadi kuanzia masaa 24. Haya ni miongoni mwa kero tunazokutana nazo wateja wa mitandao ya simu. TCRA tusaidieni wananchi, ndiyo kazi yenu kuhakikisha tunapatiwa huduma zilizo na ubora na kwa wakati.
 
nimetoka kuongea nao muda si mrefu mnajua mnanishangaza mnaosema hamuwapati!!
 
Back
Top Bottom