- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kwenye hizo audio mbili yasemekana Serikali inaidai kampuni ya Vodacom "tozo" au "kodi" kutokana na fedha zinazowekwa na wateja wake kwenye AKAUNTI ya M-Koba.
Kuna hatari Akaunti hii inaweza kusimamishwa hadi Vodacom walipe hayo mabilioni wanayodaiwa, hivyo kuathiri fedha za vikundi vilivyowekwa huko.
Maoni yangu:
Vodacom ijitokeze itoe majibu kuhusu hii Sintofahamu
Kuna hatari Akaunti hii inaweza kusimamishwa hadi Vodacom walipe hayo mabilioni wanayodaiwa, hivyo kuathiri fedha za vikundi vilivyowekwa huko.
Maoni yangu:
Vodacom ijitokeze itoe majibu kuhusu hii Sintofahamu
- Tunachokijua
- M-Koba ni njia ya kuchanga Kidigitali kwa vikundi vya VICOBA inayomuwezesha kila mwanachama kuchanga kwa usalama, urahisi na akiwa popote.
Huduma hii huendeshwa kwa ushirikiano kati ya Benki ya TCB na Mtandao wa Mawasiliano wa Vodacom.
Ikiendeshwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), na ikiwa na takriban 65% ya watumiaji ambao ni wanawake, M-Koba huwapa wanakikundi urahisi, uwazi na usalama wa kukopa na kusimamia fedha zao wenyewe wakiwa popote.
Madai ya M-Koba Kudaiwa Madeni na Serikali yaibuka
Novemba 9, 2024, ilikuwa siku ya kawaida kwenye maisha ya kimtandao kama ilivyo siku zingine hadi ilipofika jioni ambapo taarifa za Kampuni ya Vodacom kudaiwa mabilioni ya pesa (ambayo hayakujatwa kiwango chake halisi) na serikali zilianza kusambaa kwa kasi.
Hii inathibitishwa na mada hii iliyoanzishwa hapa Jukwaani ikidokeza uwepo wa hali hiyo huku ikiwataka Vodacom wajitokeze kutoa ufafanuzi. Rejea hapa.
Taarifa hii ilisambaa zaidi Novemba 10, 2024 ikihusisha pia Mitandao mingine ya Kijamii hasa X. Mathalani, watumiaji wawili wa Mtandao huo waliulizia uwepo wa sintofahamu hii. Fungua hapa na hapa kwa rejea.
Uhalisia upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia vyanzo vyake vya kuaminika kutoka ndani ya Kampuni ya Vodacom na Benki ya TCB umebaini madai haya hayana ukweli.
Pia, imebainika kuwa madai haya hayajaanza kusambaa mtandaoni mwaka huu.
Katika kuondoa sintofahamu juu ya suala hili, Benki ya TCB pamoja na Vodacom wametoa kanusho linalowataka watumiaji wa huduma hii pamoja na watanzania kwa ujumla kupuuza uzushi huo na kwamba tayari wamenza kufanya kazi na mamlaka husika kubaini chanzo chake na kuchukua hatua stahili kwa wahusika.
"Umma unashauriwa kupuuza habari za uongo na kutegemea njia rasmi za Vodacom kwa taarifa za uhakika. Vodacom pia inafanya kazi kwa karibu na mamlaka husika ili kubaini chanzo cha habari hizi za uongo na kuchukua hatua zinazostahili"
Aidha, kampuni ya Vodacom ilituma ujumbe kwa wateja wake ikiwasisitiza pia kupuuza madai hayo.
M-Koba ilianzishwa Mwaka 2019 ambapo hadi sasa imesajili vikundi takriban 375,000 huku ikiwa na watumiaji wanaofikia Milioni 2.4