Halitakuwa jambo la ajabu. 'Miss Tanzania' pageant haina mvuto wala heshima tena, kwani imetekwa na wahuni wanaoharibu tu dada zetu. Washindi wengi wanapatikana kutokana na madau ya watu wenye pesa mjini. Ingekuwa jambo la maana sana iwapo kina dada na kina mama ndani ya bunge letu waliangalie hili - wenye mandate ya kuendesha hilo hivi sasa wasipewe sole mandate ya kuendesha pageant hii bila kikomo, na badala yake tuanzishe mchakato ambapo kutakuwa na ushindani kupata mkataba husiku kuendesha hilo, ambao utakuwa reviewed kila baada ya miaka 3 au mitano, na next time you dont qualify, tupa huko. Miss Tanzania ya sasa haiendani kabisa na utamaduni wetu. Wabunge wanawake, wakisaidiana na wizara husika kama ile ya utamaduni, wanawake, na wadau wengine wanaweza rekebisha tatizo hili. Siku mkipata nafasi, kaeni chini na kina dada wanaoshiriki kwenye kitu hiki, mtasikia habari za kusikitisha sana.