Vodacom kumbe ni kero

Vodacom kumbe ni kero

Nuraty J

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
1,729
Reaction score
3,831
Wakuu habari,

Juzi nimebakisha salio la kawaida sh. 2000, leo nataka kujiunga kifurushi wananiambia salio halitoshi, naangalia Kuna sh 1900 tu.

Nawapigia Wanasema eti salio limekatwa kwajili ya huduma ya THE BEST wakati sijiungagi na huduma yoyote ya kipuuzi puuzi, yaani hii mitandao ni wezi kumbe.

Sasa hii mia mia wakikatwa wateja milioni mbili tu, si Wana mamilioni ya pesa jamani, yaani wameniharibia mood yangu leo.

BAADA YA KUWAPIGIA WAMENITUMIA MESEJI IYO

👇
Umefanikiwa kujiondoa kwenye huduma ya THE BEST. Kujisajili tena piga *149*75#
 
Hao voda hata vocha za kukwangua ukijisahau ukaiweka mezani wanaiba..
Au wanaipunguza sifuri moja, ilimradi tuu upate tabu.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Hii mitandao ina ujinga mwingi sana.Tena hii tabia yakuunganisha watu kwenye huduma zakipuuzi bila ridhaa ya watu imekithiri sana.
 
Hii mitandao ina ujinga mwingi sana.Tena hii tabia yakuunganisha watu kwenye huduma zakipuuzi bila ridhaa ya watu imekithiri sana.
Hawa dawa yao ni kuwashtaki tu, ni fursa hii vijana wapate mitaji baada ya kulipwa fidia na haya makampuni ya Simu
 
Back
Top Bottom