Vodacom M-Pesa: Tunasherehekea miaka kumi ya kubadilisha maisha ya Watanzania

Vodacom M-Pesa: Tunasherehekea miaka kumi ya kubadilisha maisha ya Watanzania

Vodacom Tanzania

Official Account
Joined
Aug 12, 2013
Posts
324
Reaction score
126
Vodacom Tanzania PLC imetimiza miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa huduma ya M-Pesa.

Kwa miaka hiyo kumi, Vodacom M-Pesa imejikita kwenye kutoa huduma mbali mbali kama kulipia huduma na bidhaa, huduma za kibenki, kuweka na kukopa pesa, kutuma pesa nje ya nchi na huduma nyingine nyingi. Huduma hizo zote zinapatikana kwa njia rahisi sana ya huduma ya pesa kwa njia ya mtandao ambayo ilikuwepo tangu mwanzoni.

Vodacom M-Pesa inaongoza Tanzania kwa huduma za kifedha za mtandao kwa makampuni ya simu za mkononi kwa asilimia 42 huku ikiwa na watumiaji hai 8.2 milioni, mawakala 106,000, wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 2,000 wafanyabiashara wadogo 15,000 na benki 30 ambao zimeunganisha kwenye mtandao wa Vodacom M-Pesa.

Kwa mtandao mpana na imara, M-Pesa imeweza kutoa huduma kwa Watanzania vijijini na mijini ambapo wameweza kutumia huduma halali ya kifedha na kusababisha kukua kwa uchumi wa Taifa kutoka 58% 2013 na 44% 2009 hadi 65% kwa mwaka 2017.
04.jpg
 
Hongereni sana.

Mjitahidi kurekebisha makosa madogo madogo yaliyopo na yanayojitokeza ili kufanya huduma iwe bora zaidi.
 
Umeandika vibaya mno....Hebu fanya editing ya ulicho andika..

Hamna para..yani umetiririka tuu
 
Mmeondoa kifurushi cha Ya kwako tu baada ya kuona maisha yetu yameboreka na uchumi umefikia 65%?
Rudisheni hicho kifurushi kuboresha huduma zenu
 
Mmeondoa kifurushi cha Ya kwako tu baada ya kuona maisha yetu yameboreka na uchumi umefikia 65%?
Rudisheni hicho kifurushi kuboresha huduma zenu
Hello Mbiirwa,
Kifurushi cha YaKwakoTu bado kipo kupitia *149*03# na kitakupa ofa kulingana na matumizi yako tu. Karibu sana
Asante
 
Mmeondoa kifurushi cha Ya kwako tu baada ya kuona maisha yetu yameboreka na uchumi umefikia 65%?
Rudisheni hicho kifurushi kuboresha huduma zenu
Acha tu. Hio nayo imeniboa kwelikweli. Nilikua napata GB 3 kwa siku 5 kwa shilingi 2000, kwa sasa wameondoa hio ofa. Majanga
 
Hello Mbiirwa,
Kifurushi cha YaKwakoTu bado kipo kupitia *149*03# na kitakupa ofa kulingana na matumizi yako tu. Karibu sana
Asante
Si maanishi mmeondoa kabisa, mmepunguza bando kutoka 1.1 GB kwa mwezi hadi 500 MB kwa wiki. sio poa kabisa, Rudisheni mmeshatunyonya sana hii miaka 10
 
Endelea kufuatilia kurasa zetu, kama ilivyo kauli mbiu yetu ya Yajayo yanafurahisha, Uko Tayari? tutakuletea mambo mazuri muda si mrefu.
Umetoa jibu kama mwana siasa.
Hapa ingependeza ukawajibu wachangiaji kwa ukweli na uwazi aiseeee
 
Hello Mbiirwa,
Kifurushi cha YaKwakoTu bado kipo kupitia *149*03# na kitakupa ofa kulingana na matumizi yako tu. Karibu sana
Asante
Mmepunguza mnooo aiseee
1000 - Mb 250
2000 - 1280
Nmewahama kwa Internet nitarudi mkirekebisha
Halaf makato yenu kwa Mpesa yamekuwa makubwa mnooo
Luku nayo bado inasumbua
 
Back
Top Bottom