Vodacom Tanzania PLC imetimiza miaka kumi tangu kuzinduliwa kwa huduma ya M-Pesa. Kwa miaka hiyo kumi, Vodacom M-Pesa imejikita kwenye kutoa huduma mbali mbali kama kulipia huduma na bidhaa, huduma za kibenki, kuweka na kukopa pesa, kutuma pesa nje ya nchi na huduma nyingine nyingi. Huduma hizo zote zinapatikana kwa njia rahisi sana ya huduma ya pesa kwa njia ya mtandao ambayo ilikuwepo tangu mwanzoni.
Vodacom M-Pesa inaongoza Tanzania kwa huduma za kifedha za mtandao kwa makampuni ya simu za mkononi kwa asilimia 42 huku ikiwa na watumiaji hai 8.2 milioni, mawakala 106,000, wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 2,000 wafanyabiashara wadogo 15,000 na benki 30 ambao zimeunganisha kwenye mtandao wa Vodacom M-Pesa. Kwa mtandao mpana na imara, M-Pesa imeweza kutoa huduma kwa Watanzania vijijini na mijini ambapo wameweza kutumia huduma halali ya kifedha na kusababisha kukua kwa uchumi wa Taifa kutoka 58% 2013 na 44% 2009 hadi 65% kwa mwaka 2017.
View attachment 789681