Vodacom m-power ni nini hasa?

Amanijua

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
1,776
Reaction score
1,619
Jamani ni almost a week now nasikia tangazo la M-PAWA kutoka vodacom na kila nikijaribu kulifuatilia nashindwa kulielewa kiufasaha.

Naombeni msaada kwa mwenye uelewa wa kutosha maana wanasema mtu anaweza kupata mikopo midogo midogo kwa ajili ya ujasiriamali kupitia line yako.
 
mkuu kama unawezaingia jf, then ningekushauri usome maelezo yao kwenye web ya vodacom wameeleza vizuri maelezo ni mengi yakutosha, kuweka hapa unaweza jaza saver, ila inaonekana iko vizuri according to maelezo yao, yaani badala ya kuacha hela kwa m-pesa unaihamishia kwa m-pawa inapata kariba kidogo then kutokana na kiwango unacho save unaweza kukopeshwa mkopo wa up to laki tano500,000 ila inatakiwa irudishwe baada ya mwezi
 
Hli nalo ni Janga.
Watumiaji wenyewe waswahili page imeandikwa kiingereza.
We mtumiaji wa kawaida atajua nini sasa hapo zaidi ya kumtia umaskini tu.
Hao wazungu pori tunaowahusudu nani atakopa hiyo pesa ndogo kama wa Elfu Moja mpala hizo laki Tano
Huu mtindo wa kampuni za simu kuchanganya watu kwa kutumia Lugha hasi ndio tatizo.
Wajipange,watu wengi hawajawaelewa na muda si mrefu malalamiko yatafuata
 
unakopa 30% ya akiba yako yani hela yako mwenyewe na kulipia riba. wanakwepa risk ya defaulting. lakini wanadai kutoa kila baada ya miezi 3? faida kwa hela utakayo save
 
piga customercare au tembelea voashop kwa maelezo zaidi. ila ukiingia kwenye ya mpesa ukienda pale namba 5 menyu ya mpawa unaelewa kila kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…