Nani amewahi kuona Terms and Agreement za hii mitandao kwa wateja wao? kama mtu anayo anaweza share hapa.
Ipo kwenye website yao check this link:
Welcome to Vodacom Tanzania
Baadhi ya terms and agreements, ziko kwa kingereza nimetafsiri.
5.8. Kwa kukubali masharti na vigezo hivi, unakubali kwamba V
odacom itakuwa inakutumia ujumbe mfupi wa maandishi kuhusu taarifa za mteja na matangazo ya bidhaa na huduma zake mara kwa mara. Ikiwa hutaki kupokea ujumbe huu, unatakiwa kuwasiliana mara moja na kituo chetu cha huduma kwa wateja au kutembelea duka lolote la Vodacom ili kusaidiwa kuondolewa kwenye huduma hizo.
6.3. Vodacom haisambazi taarifa zako binafsi kwa watu wengine (wa tatu) isipokuwa pale utakapoomba wewe mwenyewe, au pale ambapo inahitajika kisheria kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria. Kwa ajili ya kuepuka mkanganyiko na kwa uwazi zaidi, Vodacom inaweza kulazimika kufichua taarifa binafsi ili kutimiza masharti ya kisheria au ya udhibiti kwa mujibu wa sheria husika.
6.5. Ufuatiliaji au kurekodi mawasiliano yako kama vile simu au ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) unaweza kufanyika kama inavyotakiwa kisheria au kwa madhumuni ya kibiashara kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria. Hata hivyo, katika hali hizi, hatutafichua taarifa zozote ambazo zinaweza kutumika kukutambua moja kwa moja kama mtu binafsi.