Vodacom na mitandao mingine zuieni sms za Tume ya Uchaguzi ni kero kwa watanzania

Vodacom na mitandao mingine zuieni sms za Tume ya Uchaguzi ni kero kwa watanzania

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Ni jambo la kushangaza na kusikitisha kuona Watanzania wengi wakilalamika kuhusu wimbi la jumbe zinazotumwa kila siku zikiwa na ujumbe wa “Jitokeze kupiga kura tarehe 29 Oktoba 2025 kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani. Kura yako ni haki yako.”

Wengi wanasema ujumbe huo, unaoonekana kama kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha upigaji kura, umegeuka kero badala ya kuwa elimu.


images (3).png

Malalamiko yamezidi mitandaoni, ambapo baadhi ya wananchi wanasema wanapokea zaidi ya ujumbe mmoja kwa siku kutoka kwa mitandao tofauti, jambo linaloleta usumbufu mkubwa.

Mdau mmoja aliyejaribu kuwasiliana na huduma kwa wateja wa Vodacom alidaiwa kuelezwa kuwa jumbe hizo zinatoka kwa Tume ya Uchaguzi kwa ushirikiano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Swali kuu linabaki: je, TCRA inapaswa kuruhusu ujumbe wa aina hii bila ridhaa ya watumiaji? Wengi wanahoji kama mamlaka hiyo inatambua athari za usumbufu wa kidijitali, hasa kwa wale wanaotaka faragha. Wengine wanadai jumbe hizo zimeanza kufanana na zile za utapeli mtandaoni, zinazotumia namba zisizojulikana.
 
Back
Top Bottom