Vodacom nani aliyewaruhusu kuwapa CCM namba yangu ya simu?

Vodacom nani aliyewaruhusu kuwapa CCM namba yangu ya simu?

Binafsi sijaona tatizo kupata meseji za vyama tofauti tofauti kwani hata Nchi zilizo endelea hawatangazi kwenye magari barabarani ya kupigia watu kelele wakichapa kazi
Badala yake hutumia TV, Twitter, sms na njia mbalimbali mbadala za kielekroniki kuwasiliana na watu
Matangazo na hasa usiku ni kero! Muziki sauti kubwa sana.
 
Hapo ndo wamekuja kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka.
 
Binafsi sijaona tatizo kupata meseji za vyama tofauti tofauti kwani hata Nchi zilizo endelea hawatangazi kwenye magari barabarani ya kupigia watu kelele wakichapa kazi
Badala yake hutumia TV, Twitter, sms na njia mbalimbali mbadala za kielekroniki kuwasiliana na watu
Tatizo lipo unatoaje namba ya mtu kwa chama cha siasa bila ruhusa yake, CCM sio polisi na hawana order ya mahakama kuchukua na kutumia au kufuatilia namba yangu kilichofanyika hapa ni kosa hakuna kupindisha, mazoea hayawezi fanya kosa likawa sio kosa.
 
Mi nimepokea pia kupitia voda japo sio mgombea wa kijani.
 
Nimeshakaa kwenye mtandao hapa nasubiri wanitumie tu, hakika watanipa fungu zuri sana la kunifanya nipumzike hata miaka mitatu bila kuumiza kichwa.
 
Ndugu Mwananchi, Mimi John Pombe Joseph Magufuli, mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, kwa heshima na unyenyekevu mkubwa, ninaomba kura yako ya NDIYO kwangu, Mbunge na Diwani wa CCM ifikapo tarehe 28/10/2020, Tumetekeleza kwa kishindo tunasonga mbele pamoja. Asante sana na Mungu akubariki.

Nitachukua hatua zaidi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Airtel hii kitu haijafanywa wala tiGo. Sasa naamini kuwa Voda ni mtandao wa Chama
 
Hali ni tete sana Pale CCM makao makuu.
Tathmini ya kikao cha siri cha jana inasemekana ripoti zinasema maji yamezidi unga na kuni za kuchochea moto zimekuwa majivu. Kila silaha sasa inaingizwa vitani.

Hakuna kikao kilichofanyika jana. Wala hakuna kikao cha Siri.
-
Mimi binafsi ningependa sana kukufahamu nje ya JF!
 
Hivi ukishapokea huo ujumbe system inaruhusu reply?
Hairuhusu halafu kwa uelewa wangu ni kwamba sio kila mtu anapata hyo msg nafikiri ukitajwa na jina lazima uwe na connection flan labda una kadi ambayo ulijisajili kama mwanachama halali si kwamba zimetumwa randomly
 
Nimeshakaa kwenye mtandao hapa nasubiri wanitumie tu, hakika watanipa fungu zuri sana la kunifanya nipumzike hata miaka mitatu bila kuumiza kichwa.
Broo, ukiamka kutoka kwenye huu isingizi nenda kanywe chai. Usipige mswaki. Zingatia masharti achana na vigezo
 
Back
Top Bottom