Vodacom ni wezi na mmenikosanisha na Wateja,

lup

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
2,514
Reaction score
2,741
Za mchana huu wadau..pamoja na sifa walizonazo lakini pia Mna sifa ya wizi kwa Wateja wenu
Kisa ni hiki; asubuhi kaja mteja dukani kwangu akataka nimuweke vocha na nimuunganishie kifurushi..nikaweka vocha,Mara ya kwanza nikajibiwa kuna tatizo nijaribu baadaye,nikaweka tena nikajibiwa vicha haipo,nikweka kwa Mara ya tatu nikajibiwa imetumika kwenye namba inayoishia namba ya mteja yule ninayemuwekea, nikanunua kifurushi.nikajibiwa sina Salio lakutosha,kuangalia Salio ni 0.25 kuwapigia Huduma kwa Wateja wakasema nikweli vocha imeingia lakini imetumika ila record haionekani,mteja wangu anadai hana deni,hajajiunga ni Huduma yoyote sasa iweje vocha yake itumike..mteja akaanza kunifokea Mimi nakuhisi Mimi ndio nimeitumia vibaya au nimemuibia....
Kisa cha pili, huwa naweka Salio bila kujiunga kifurushi cha ajabu ikipita Siku bila Kujiunga huwa nakuta Salio limekatwa tayari na kuniingiza hasara tens..
Nilifikili ni mimi tu,nimemuuliza mdogo wangu naye anasema huwa anakuta Salio limepungua sh.5 bila matumizi
YAANI VODA NASEMA HUO NI WIZI KAMA ULIVYO WIZI MWINGINE NA MNAKERA SANA
 
Leo kulikuwa na tatizo mkuu hata mimi nimekutana nayo hiyo
 
Nashangaa natumiwaga meseji sijui kuna mtu kashinda million 150 lakini jina hawalitaji....mara ukitaka kua millionea cheza kwa Tshs. 300....shenz kabisa hawa Vodacom
 
Mimi pia nashangaa naweka salio kwa ajili ya kuangalia balance ya benki lakini hata nikiweka 1000 nitatumia mara moja tu. Nikitaka kutumia kiasi hicho hicho kuangalia mara ya pili,naambiwa sina salio. Kwa kweli Voda wametuchosha kwa wizi huu
 
Nimewahi kukutana na changamoto kama hiyo ila kwa Air tel.

Naingiza vocha inaniambia EXTERNAL APPLICATON DOWN...na ikishakwambia hivyo ndio basi tena ukirudia kuingiza hiyo vocha inakwambia vocha imeshatumika......kuna kipindi nimepigwa sana, ila kwa sasa naona imetulia.
 
Hao voda majambazi sana, ila hata tgo wana tabia hyo ukiweka salio ukachelewa kujiiunga imekula kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…