Vodacom ni Wezi?

Yaani sometime wanatuma msg eti bado mb 150, unaamua kuzimansata na kusign out insta kupunguza matumizi. The ushazima.data unaambia kifurushi kimeisha

hiyo sms huwa haina maana ni kama pale mwanaume anamwambia demu mpira umepasuka[emoji23][emoji23][emoji23]huwa kashafunga goli.
 
jamani msisahau google photo kama umeweka backups ukiunga mb tu ina upload picha,so bundle linayoyoma tu.
 
jamani msisahau google photo kama umeweka backups ukiunga mb tu ina upload picha,so bundle linayoyoma tu.
Acha walalamike. Wakati wamesett app zao ziji update automatically wanapofungua data .
 
Umefungaje data na mtandao unasoma 4g
Hujawahi kutumia simu za 4g wewe, ukifunga data 4g inasimama kwenye mtandao bila kucheza but ukifungua data ndipo 4g inaanzs kupanda na kushuka. Najua hujawah kuzitumia ndio maana umeshangaa. Ukiangalia hiyo 4g imesimama tu kwenye mtandao, tafsiri yake ni data zipo off mkuu. Hope umenielewa.
 
Nikisimamisha data hata hizo ma4g hazisomi. Nawajaribu voda hapa nimenunua cha 550MB nataka nibrowse tu jamiiforum, watsapp nione nitadumu kwa muda gani.
 
VODACOM tabia ya kuiba mabando ya internet wanayomuda mrefu sana, ndio maana nimewakimbia. Kwanza gharama zao ni kubwa mno. Nipo zangu zantel sitaki tabu 4g ya maana na ni cheaper japo wamepandisha gharama majuzi ila bado ni nafuu kulinganisha na hawa ngumbaru wezi. Na usiombe customer care akapokea mwanamke yani unaweza pasua simu, hawajui technicalities wao ni majibu kama robot tu.
 
Voda wanatafuna bundle hilo halina utani. Mimi natumia tigo miaka yote nikiweka voda kifurushi labda tigo mtandao uwe chini.

Nina ttcl pia internet yao iko vizuri na uzuri inafanya roaming na tigo japo naitumia kama hotspot home
 
Wewe nawe bado uko na voda tu ? Wengine tulishaachana nao kitambo. Ni wapuuzi sana. Voda naitumia kwa miamala ya fedha tu basi
 
Sawa mfanyakazi wa voda.
Lakini mwenzio nilimpigia simu nikamuuliza nimejiunga saa ngapi akasema saa 1na dakika 47.
nikamwambia baada ya kufungua data nikaingia jf nikafunga data nikalala saa 9 usiku naamka nafungua data naingia Instagram dakika 3 nyingi mnanitumia meseji data zimeisha.MB 550 zimeishaje?
Akaanza kujiuma uma
Nikamwambia nyie ni wezi,tena majambazi na waambie na mabosi zako "MBWA NYIE"
nikakata simu.
NARUDI HALOTEL
 
Dah! Sawa mi mwizi na mimi ni mfanyakazi wa Vodacom..😅
 
Lugha ya malkia Mimi siiweziiii [emoji1787]
 
Nanunuaga ya 2000 GB 1.5 kwa siku tatu lakini simalizi siku2 imakekata. Masaa24 mengi ikizidi sana 28. Nilikuwa halotel nkaenda voda.. Nimetua airtel . sa sijui tukimbilie wapi
Ahahah sehemu ya kutulia ni Halotel. Mb zao unadumu nazo muda mrefu. Lkn mtandao utajua mwenyewe pa kuupata. Bs shida tupu
 
Ili nalo Lina ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…