Vodacom Premier League, Simba SC 3-3 Stand United Uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam

Vodacom Premier League, Simba SC 3-3 Stand United Uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara (VPL,) kuendelea leo katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam, ambapo vinara wa ligi hiyo Simba SC kuwakaribisha Chama la Wana, Stand United kutoka Shinyanga.

Ni Mchezo mkali wa kukata na shoka. Je Simba SC wataendeleza vimbi la ushindi? Au Stand United watavunja mwiko wa vinara hao kutopoteza mchezo wowote kwenye ligi kuu ya VPL?

Kumbuka patashika hii itakuwa mubashara na Azam Sports 2 na upande wa redio TBC Taifa itapeperusha matangazo hayo kuanzia saa 10: 00 jioni. Usikose ukaambiwa kuwa nasi hadi mwisho.
9b133e217b39ca692f10bb880509e079.jpg
8b2f23345154e216ef75b0982de7af7c.jpg


Vikosi vya mchezo wa leo kwa pande zote mbili, Simba SC Vs Stand United hivi hapa.
3cb9dc9ca07056be54e3e53c5f69997b.jpg


=>00' Naam mpira umeanza hapa uwanja wa Taifa.

Simba SC 0-0 Stand United

07' Goooooooooaaal Asante Kwasiii anaindikia Simba bao la kwanza baada ya golikipa kutema shuti la Mavugo

Simba SC 1-0 Stand United

15 ' Simba wako mbele ya goli moja dhidi ya Stand United.

Goooooooooaaal. Mavugo anaandika bao la pili. Kazi mzuri kutoka kwa Shomari Kapombe

Stand United toka mwanzo wameanza kujilinda hivyo kutoa fursa Simba kutawala mchezo huu

35' Mavugo anajaribu kuwatoka mabeki wa Simba. Lakini ni Offside.

Stand United wanashambulia lango la Simba hapa dakika hizi..lolote linaweza kutokea

36 ' Gooooaaal.. Stand United wanapata bao kusawazisha kupitia Kwa Tariq Seif baada gonga safi kwa wachezaji wa Stend United.

86' Konaaaaa Gooooaaal, ilipigwa kona na Lulambo na kwenda moja kwa moja na kuandika bao la pili upande wa Stand United

Simba SC 2-2 Stand United

45' Za kipindi cha kwanza za mchezo wa VPL zimekamilika hapa uwanja wa Taifa ambapo. Timu zote zikitoshana nguvu kwa magoli mawili kwa mawili. Simba SC 2-2 Stand United

=>Mpira umeanza 45 ' za kipindi cha pili uwanja wa Taifa Simba SC dhidi ya Stand United. Ambapo Simba SC wamemtoa Mavugo na nafasi yake kaingia Luizio

56' Kichuyaaaaaaa anapiga shuti na golikipa anaokoa. Ilikuwa nafasi nzuri kwa Simba SC

63' Goooooooooaaal.. Gooooaaal Simba wanaandika bao la tatu baada ya mpira wa kona uliokolewa na golikipa kumkuta Nicholas Gyan na kupiga shuti kali na kutinga wavuni. Simba SC 3-2 Stand United

66' Goooooooooaaal. Stand wanaandika bao la tatu kupitia Kwa Blaise shuti kali baada ya mpira uliokuwa ukielekea lango la Simba, mabeki kushindwa kuokoa hatari hiyo

Simba SC 3-3 Stand United

74' Simba wanafanya mabadiliko. Anaingia Kazimoto na anatoka Mzamir Yasin

Pamoja na Simba kutawala mchezo bado mashambulizi ni makali kwa pande zote mbili.. Kuelekea kumalizika kwa mtanange huu

89 ' uwanja wa Taifa Dar es salaam. Simba SC 3-3 Stand United

90+4' za mchezo wa mpira wa ligi kuu VPL. Simba SC 3-3 Stand United.

=> Naam dakika 90' za mtanange wa soka wa Vodacom Premier League kati Simba SC dhidi ya Stand United zimekwisha uwanja wa Taifa. Ambapo timu zote zimetoshana nguvu kwa kila timu kupata mabao matatu.

Simba SC 3-3 Stand United.
d2b05e37bc243ca025d36b8996251d16.jpg
604a98fdd582a51de31c745f6f9d9f00.jpg
f556ea48e605ed1bd99e3f908ca5503f.jpg


==>Asanteniiiii sana wakuu wako.... Ghazwat
 
Hivi hawa makocha na viongozi wanatutaka nini mashabiki wa simba? Huyo mavugo wao hana nguvu, hana purukushani kabisa kwa mabeki wa timu pinzani pia huwa hakabi kabisa kuanzia mbele kama boko na okwi wanavyofanya kwa nini wasimpange kitandu huyo dogo wa timu B. mfano mzuri ni mechi ya mwadui lakini kwa nini hawataki kujifunza. huyo kitandu ana nguvu na anaweza kupambana na mabeki kibongo bongo walau itawazuia mabeki wa stand wasiongeze nguvu kwa washambuliaji wao. Yaani leo sijui itakuwaje ngoja tuone dakika tisini zitaishaje.
 
Mpira umeanza kwa taratibu hapa hapa uwanja wa Taifa.

Simba SC 0-0 Stand United
 
5' hakuna timu imepata bao mpaka sasa, mashambulizi ni kwa pande zote
 
7' Goooooooooaaal Asante Kwasiii anaindikia Simba bao la kwanza baada ya golikipa kutema shuti la Mavugo.
 
10 ' bado Simba wako mbele ya goli moja
 
Back
Top Bottom