Vodacom Premier League, Simba Sports Club yatoka sare na Lipuli FC uwanja wa Uhuru 26/11/2017

Vodacom Premier League, Simba Sports Club yatoka sare na Lipuli FC uwanja wa Uhuru 26/11/2017

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya ligi kuu ya Vodacom Premier League (VPL) inaendelea leo Jumapili katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, ambapo Simba SC Wekundu wa Msimbazi wakipimana ubavu na Lipuli FC wana Paluhengo.

Nani kuondoka na pointi 3 muhimu? Lipuli inafundishwa na Suleimani Matola na Amri Said ambao wamewahi kucheza klabu ya Simba SC kwa mafanikio. Na Simba chini ya Omog. Usikose ukaambiwa, anadamana nami hadi tamati.

Kumbuka mechi hii itakuwa mubashara kupitia Azam Sports 2 na kwa upande wa radio TBC Taifa itapeperusha matangazo hayo kuanzia saa 10. 00 jioni.

Vikosi vya timu kwa upande Simba Sports Club ambao ni wenyeji wa mchezo huu;

Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Yussuf Mlipili, James Kotei, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassir, John Bocco, Mwinyi Kazimoto, Haruna Niyonzima.

Sub;

Emmanuel Mseja, Ally Shomari, Jamali Mwambeleko, Method Mwanjale, Nicolas Gyan, Laudit Mavugo, Juma Luizio.

Kwa upande wa Lipuli FC ambao ni wageni katika mchezo huu;

Agathon Mkwando, Hussein Rashid, Ally Mtoni, Joseph Owino, Asante Kwasi, Hamad Manzi, Seif Rashid, Mussa Nampaka, Ramadhani Mandebe, Malimi Busungu, Shaban Ada.

Sub;

Mohamed Yusuf, Novalty Lufunga, Martin Kazila, Neoka Shaban, Waziri Ramadhani, Tola Anthony, Omega Same.

=>Mpira umeanza hapa uwanja wa Uhuru

1' Simba SC 0-0 Lipuli FC


15: Go Go Goooooooooaal, Mwinyi Kazimoto anaiandikia Simba bao la kwanza.

Simba SC 1-0 Lipuli FC


19 ' Goooooooooaal.. Mpira wa adhabu ulipigwa moja kwa moja na Asante Kwasi unahesabu goli la kusawazisha kwa Lipuli FC .

Simba SC 1-1 Lipuli FC

30' ya mpambano wa mpira hapa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam

Simba SC 1-1 Lipuli FC

45 ' Naam mpira ni mapumziko hapa uwanja wa Uhuru. Ambapo timu zote zimetoshana nguvu kwa matokeo ya goli moja kwa moja

Simba SC 1-1 Lipuli FC

46' Mpira umeanza kipindi cha pili hapa uwanja wa Uhuru

70' Simba SC 1-1 Lipuli FC uwanja wa Uhuru

90+5 ' Mpira umekwisha hapa uwanja wa Uhuru, ambapo timu zote zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya goli moja kwa moja, ambapo Simba wakitangulia kufunga kupitia kwa Kiungo Mwinyi Kazimoto 15' na 19' Asante Kwasi akisawazisha bao hilo kwa mpira wa adhabu.

Simba Sports Club 1-1 Lipuli FC
 
Gooooooo Smb 3 lpl 0

Okwi dk 3
Okwi dk 10
Kichuya dk 45

HT
 
3' Bocco oooo unagonga mwamba nje!
 
9' Kichuyaaaaa kona hapa, inapigwa konaaaaa nje
 
10' mpira ni mkali uwanja wa Uhuru ambapo Simba wanashambulia vikali hapa huku Lipuli wakiwa bado kufika lango la upinzani
 
15 'Kazimoto goooooooooaal, Simba wanahesabu bao la kwanza

Simba SC 1-0 Lipuli FC
 
4 tu zinawatosha hawa. Tujikite zaidi kileleni.

upload_2017-11-26_16-17-34.png
 
Back
Top Bottom