Vodacom Premier League 'VPL' Alliance FC Vs Simba SC, Furaha Kwa Wanasimba Uwanja wa Kirumba

10' Hakuna bao milango bado ni migumu, kumbuka matangazo haya yanakujia kwa hisani ya team JF

Alliance FC 0-0 Simba SC
 
Dilunga aaaaaaa, doooooh, anakosa nafasi ya wazi, ilikuwa yeye na golikipa ambapo mpira wake umepaaa juu ya lango.
 
15' Alliance FC wamelifikia lango la Simba mara tatu, huku wakishambuliwa sana na Simba, kama hali itakuwa hivi kuna uwezekano wa Simba kupata bao.

Alliance FC 0-0 Simba SC
 
Simba wanahitaji utulivu mbele ili waweze kupata bao, kwani wamepata kona 4 ambazo hazikuzaa matunda

24' Alliance FC bila Simba bila
 
Umilikiwa wa mpira kwa Simba SC 70% kwa 30% Alliance FC, huku Alliance wakipata free kick

28' Inapigwaaaaaa goooooooooooal
Alliance FC wanaandika bao la kwanza

Alliance FC 1-0 Simba SC
 
38' Kocha Sven Vanderbroeck anatakiwa afanyie kazi kuhusu mipira ya free kick na Kona, zimepigwa kona takriban 5 lakini hakuna matunda
 
Anakwenda mchezaji wa Alliance anafumua shutiiiiiiiiii, njeeeeeeee

Wanachokifanya wakipata nafasi wao wanapiga tu langoni, hii plan huenda ikawasaidia
 
45+3' kuelekea kuwa mapumziko huku Alliance FC wakitangulia bao moja

Wanakwenda Simba, hatari langoni mwa Alliance, anapigaaaaaa anakosaaaa

Ni free kick kuelekea lango la Alliance, inapigwaaaaaa kwake Shiboub, kwake Mkudeeeeeeee

Goooooooooooooooooooaaal

Goooooooooooooooooooaaal

Jonas Mkude anaisawazishia Simba SC, na sasa ni mapumziko

HT: Alliance FC 1-1 Simba SC
 
Mbona mmesusa kuleta updates
 
Goooooooal nani sasa kapigwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…