Vodacom Premier League VPL' Lipuli FC dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Samora Iringa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Naaam...bila shaka wote hamjambo kabisa, na nasema Amani iwe kwenu Mungu Awatangulie..!

Ni Jumamosi nyingine ya February 15, 2020 ambapo nyasi kwenye viwanja mbalimbali kuwaka moto katika patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL).

Kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa, Wenyeji Lipuli FC, Wanapaluhengo, Wanamkaribisha Mfalme wa Nyika, Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni, Simba SC, mchezo ambao unatabiriwa kuwa mkali na wa kusisimu kwa muda wote wa dakika 90, kusaka alama tatu muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo wa VPL.

Kocha wa Lipuli FC Julio Helieza amesema wanaiheshimu Simba SC ni timu kubwa na zoefu, lakini wakiwa nyumbani wamejiandaa kwa lengo la kupambana kwa nguvu zote kuona wanaibuka na ushindi.

Naye Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck, amesema lazima wacheze mchezo katika kila hali ambayo wanakutana nayo, hivyo wamejiandaa vya kutosha kwa hilo kuhakikisha wanafanya vizuri, kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo.

Nani kuibuka na furaha ya ushindi?Tusubiri dakika 90 za mchezo..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 jioni, Usikose Ukaambiwa.
 
Muda mchache mtanange utaanza uwanja wa Samora..!

Naaaaaaam mpira umeanza ni patashika ya kukata na soka mfululizo wa VPL

Lipuli FC 0-0 Simba SC
 
05' mashambulizi ni makali kwa pande zote, ambapo Lipuli walipata kona ambayo haikuzaa bao
 
Chamaa anakwendaa, anapigaaa lakini mlinzi Lufunga anaokoa mchomo wa Chama na kuwa kona ambayo haikuzaa bao

Ilikuwa jaribio kali kwa Simba SC..!
 
Masumbukoooo, lakini golikipa Manula anaruka na kuondosha hatari ile laaaaah

Ilikuwa nafasi kwa Lipuli FC kuandika bao
 
12' Milango ni mugumu Uwanja wa Samora..VPL

Lipuli FC 0-0 Simba SC
 
18' Mchezo ni mkali huku timu zinashambuliana kwa zamu huku Simba wakitawala eneo la ushambuliaji kuliko Lipuli FC

Lipuli FC 0-0 Simba SC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…