Vodacom Premier League 'VPL' Mbao FC dhidi ya Simba SC, Uwanja wa CCM Kirumba

Vodacom Premier League 'VPL' Mbao FC dhidi ya Simba SC, Uwanja wa CCM Kirumba

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya ligi kuu Tanzania Kuendelea kupigwa leo January 16, 2020 kunako Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Mbao FC wakiwa nyumbani wanawakaribisha Mabingwa wa Nchi Simba SC.

Mchezo unatarajiwa kuwa mkali na wa vuta nikuvute kwa muda wote wa mchezo na hasa kila timu kuhitaji alama tatu muhimu ili kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania VPL.

Kumbuka mchezo utaanza saa 10:00 jioni..Usikose Ukaambiwa

•••••••========•••••

Mchezo wa VPL kati ya Mbao FC na Simba SC umekwisha uwanja wa CCM Kirumba ambapo Simba wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Mbao FC

Simba SC ndo walikuwa wa kwanza kupata bao kunako dakika ya 42' likifungwa na Hassan Dilunga, na Jonas Mkude dakika 47' huku lile la Mbao FC likifungwa na Wazir Junior dakika ya 53'

Kwa matokeo hayo Simba wamejikita kileleni wakikusanya alama 38. wakiwa wamecheza michezo 15.

FT: Mbao FC [emoji460] 1- [emoji460][emoji460] 2 Simba SC

...Ghazwat

tapatalk_1579178834311.jpeg
IMG_20200116_154747_819.jpeg
 
Wakati wowote mpira utaanza dimba la Kirumba

Naaaaaaaaaaaaaaam mpira umeanza VPL, Mbao FC Vs Simba SC
 
05' mchezo umeanza kwa kasi Simba wakipata kona ambayo haikuzaa matunda, huku hali ya uwanja wa Kirumba siyo ya kuridhisha kutokana baadhi ya sehemu kuwa na maji kutokana na mvua

Mbao FC 0-0 Simba SC
 
Simba taifa kubwa, chapa hao wauza mbao wa ilemela tatu bin sufuri.
 
28' bado mpira ni mgumu kwa pande zote mbili kwa maana hakuna bao huku Simba wakipata faulo baada mchezaji wa mbao kuunawa mpira eneo la hatari

Inapigwaaaaaa na Chamaaa inagonga ukuta wa mabeki wa Mbao FC
 
Back
Top Bottom