Vodacom Premier League VPL' Simba SC dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa

Vodacom Premier League VPL' Simba SC dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Taifa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Hello Tanzania na Kote Duniani...!

Naaam mwendelezo wa patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL, kuvurumishwa leo February 18, 2020 ambapo Mfalme wa Nyika, Mnyama Mkali, Simba SC anakwaruzana na Kagera Sugar kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo utakuwa mkali, na wa kusisimua kwa muda wote wa mchezo kutokana na mbinu kwa pande zote mbili kutoka kwa makocha wake..!

Kocha wa Simba Sven Vanderbroeck kikosi chake kimejiandaa vizuri kuhakikisha mashabiki wa Simba soka safi pamoja na ushindi wa alama tatu muhimu kwa mchezo wa leo.

Naye kocha wa Kagera Mecky Mexime, anasema mchezo utakuwa mgumu na wa ushindani Simba wapo vizuri hata hivyo wamejiandaa vizuri na wanaifahamu Simba na namna ya kuikabili ili kupata ushindi.

Wanasimba na Mdau wa Kandanda nini kitatokea uwanja wa Taifa? Kumbuka mchezo ni saa 1:00 usiku Usikose Ukaambiwa.
IMG_20200218_181454_699.jpeg
IMG_20200218_181911_806.jpeg
 
Mungu ibariki Simba Sports Club Mnyama mkali kabisa msituni
Najua kagera Watakuja wamepania Ila nawaamini chama langu hamuwezi kutuangusha

Baada ya draw yao Leo nategemea usiku kutakua kuna VAR za kutosha ili wajisahaulishe draw yao

Maana Leo Wachezaji wa simba wakipiga hata danadana Tutegemee malalamiko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnyama mkali Simba sc tafuna hao Kagera sugar

Simba nguvu moja
Simba bingwa 2019/2020
 
Hiki kikosi ni cha kucheza na Tp Mazembe kabisa sio cha Kagera sugar
 
05' Mpira umeanza kwa kasi, ambapo simba wamelifikia lango la Kagera mara mbili huku wakipata kona ambayo haikuzaa bao

Wanakwenda Simba kwake Bocoo anaruka juu laaa mpira unagonga mwamba..ilikuwa hatari
 
10' game ni kali huku mashambulizi yekielekezwa sana upande wa Kagera Sugar

Anakwenda kwake Luis, anampasia Boco, anampa Kagereeee anapigaaa shutiiiiiii golikipa Tinocco anacheza vizur na kuokoa hatari ile

VPL, Simba SC 0-0 Kagera Sugar
 
Wanakwenda Kagera, lakini Mohamed anatokea na kulala kuondosha hatari..

Wanamiliki simba kwake bocco pembeni, anapiga cheka, anapenyeza kwake Chamaaa, lakini refa anasema Chama aliunawa mpira
 
Back
Top Bottom