Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Uhuru

Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Uhuru

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Kuelekea kulisaka taji la Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL, mabingwa watetezi Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, leo Alhamisi Novemba 7, 2019 anaingia kwenye dimba la uwanja wa Uhuru kukipiga na Wajelajela Tanzania Prisons.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na wa vuta nikuvute kwa muda wote wa dakika tisini hasa ukizingatia kwamba Simba SC anaingia kwa nia moja tu ya kuhakikisha anakusanya alama tatu muhimu ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa VPL.

Je Tanzania Prisons watakubali kuachia alama tatu mbele ya Mnyama Mkali Simba, au Simba SC ataendelea kuonyesha kuwa yeye ni mwamba wa soka Tanzania?

Usikose Ukaambiwa...Kuanzia saa 10:00 Jioni.

•••Kulitaka Mwana..Kulipewa Mwana..NguvuMoja

IMG_20191107_153802_353.jpeg
IMG_20191107_153819_819.jpeg
 
Naaaaaaaam mpira umeanza Uwanja wa Uhuru, mtanange wa VPL kati ya wenyeji Simba SC na wageni Tanzania Prisons

Simba SC 0-0 Tanzania Prisons
 
03' Simba SC wamepata kona mbili mfululizo ambazo hazikuleta matunda kwa kuokolewa na mabeki wa Prisons
 
10' Ajibu anapiga free kick, lakini mpira unatoka nje ya lango la Tanzania Prisons

Simba SC 0-0 Tanzania Prisons
 
15' Salim Kimenya wa Tanzania Prisons anakosa bao, mita chache kutoka lango la Simba SC, ilikuwa hatari sana..!
 
20' Simba wako upande wa Kaskazini wakipeleka mashambulizi upande wa Kusini...milango bado ni migumu hapa uwanja wa Uhuru

Simba SC 0-0 Tanzania Prisons
 
22' Free kick anakwenda kupiga Chama, inapigwaaaaa lakini golikipa anaokoa na yupo chini baada ya kupata rabsha.
 
27' milango ni migumu wakati Kapombe akiambaa ambaa na mpira pembeni mwa uwanja na mpira unadhibitiwa

Simba SC 0-0 Tanzania Prisons
 
Asante mwalimu kashasha nakusoma kwa uzuri kabisa kupitia 88.3 jamii fm
 
Back
Top Bottom