Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC Vs Lipuli FC Uwanja wa Uhuru, Ushindi Pamoja na Burudani

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Naaaaaaam! Salaam Tanzania na duniani kote..

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania VPL kuendelea kupigwa leo Desemba 25, 2019 kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam ambapo Mabingwa wa Nchi, Simba SC Mnyama Mkali kuliko Wote Mwituni, wanawakaribisha Lipuli FC, Wanapaluhengo kutoka mkoani Iringa

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90' kutokana na rekodi baina yao inayozidi kuongeza ushindani wa mchezo, kwa rekodi za hivi karibuni, wamekutana mara nne, ambapo February 26 mwaka huu, Simba SC walishinda 3-1 na mechi nyingine wakitoka sare ya 1-1 mara mbili na moja wakitoka suluhu 0-0.

Kocha msaidizi wa Simba SC, Suleimani Matola, amesema wamejipanda kuhakikisha wanapata ushindi ili kukusanya alama tatu muhimu, huku Kocha wa Lipuli akijibu kwa kusema wako tayari kupambana na Mnyama Simba.

Kumbuka mtanange huu, utaanza saa 10:00 jioni, Usikose Ukaambiwa..!



•••••••===========•••••••••

Mchezo wa VPL kati ya Simba SC dhidi ya Lipuli FC, umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao manne bila majibu yakifungwa na Francis Kahata 11' Maddie Kagere 49' na Hassan Dilunga 57'p 65, za mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Kwa matokeo hayo timu ya Simba SC imeendelea kujikita kileleni kwa kujikusanyia alama 28 kwa michezo 11.

FT: Simba SC 4-0 Lipuli FC
 
Leo kama una hela kama Simba SC basi kwako ni sikukuu..ila kama huna hela kama Gongowazi kwako ni Jumatano..!NguvuMoja
 
Wachezaji wa Simba SC wakipasha misuli kabla ya mchezo kuanza NguvuMoja
 
00' Wakati wowote mpira utaanza kupigwa uwanja wa Uhuru

Naaaaaaam mpira umeanza VPL
Simba SC Vs Lipuli FC
 
05' mpira umeanza kwa kasi kwa mashambulizi kwa pande zote, Simba wakifika mara tatu lango la Lipuli dhidi ya mara moja

Simba SC 0-0 Lipuli FC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…