Vodacom Premier League VPL | Simba SC Vs Mbeya City (4-1) | Benjamin Mkapa

Vodacom Premier League VPL | Simba SC Vs Mbeya City (4-1) | Benjamin Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Kuendelea kupigwa leo Juni 22 2021, ambapo Mabingwa wa Nchi wanawakabili Mbeya City Uwanja wa Benjamin Mkapa Jiji Dar es salaam.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mkali na wakusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu ikihitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sawa kwenye msimamo wa VPL.

Simba SC ambao ndo Vinara wa VPL wakiwa na alama 70 wanawakabili Mbeya City waliopo nafasi ya 13 wakiwa na alama 36 ambapo leo City wanaingia dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza wa 1-0 kwenye Uwanja wa Sokoine.

Je Simba SC ataendeleza ubabe wake au Mbeya City atakataa uteja? Dakika 90 kuamua. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku Usikose Ukasimuliwa.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
..... Ghazwat......


================

Timu zipo uwanjani zikifanyiwa ukaguzi salamu pamoja na kupiga picha za kumbukumbu. Kuashiria kuanza kwa Kandanda.

00' Naaaam mpira umeanza dakika 90 za jasho na damu Uwanja wa Mkapa | Simba SC 0-0 Mbeya City

05' Hakuna timu imeona lango la mwenzake huku Simba SC wakikosa nafasi ya kufunga baada ya Miquissone shutiiiiii lake kutoka nje na kuwa goal kick.

15' Simba wamepata Kona mbili ambazo haikuzaa matunda baada ya mabeki wa City kuokoa hatari zote hivyo kuweka ugumu wa mchezo huu | Simba SC 0-0 Mbeya City.

20' Mchezo ni mkali kosa za hapa na pale huku Simba wakimiliki zaidi mpira kuliko Mbeya City | Simba SC 0-0 Mbeya City

30' Bwalya Goooooooooaaal Goooooooaaal

Rally Bwalya anaipatia Simba SC bao la kwanza kwa shutiiiiii kali likimuacha golikipa Mandanda akiruka bila mafanikio | Simba SC 1-0 Mbeya City.

Simba SC walisakama lango la Mbeya City huku City wakizuia lango.

Anakwendaa Miquissone anapiga shutiiiiii Goooooooooaaal Goooooooaaal

Luis Miquissone anaipatia Simba SC bao la pili kwa shutiiiiii | Simba SC 2-0 Mbeya City.

Mbeya City wanamjaribu Kakolanya kwa shutiiiiii kali mbali, lakini anadaka.
Kapombe yupo chini baada ya kupata rabsha ameinuka mpira unaendelea.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko Uwanja wa Mkapa. Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Simba wapo mbele kwa mabao mawili kwa bila.

VPL, HT: Simba SC 2-0 Mbeya City


Kipindi cha lala kwa buriani kimeanza huku kukiwa hakuna mabadiliko kwa pande zote mbili.

46' Goooooooooaaal Goooooooaaal Bocco anahesabu bao la tatu akipokea pasi murua kutoka kwa Hussein | Simba SC 3-0 Mbeya City.

City wanajenga mashambulizi kuelekea Simba hatariiiiiii

50' Goooooooooaaal Goooooooaaal. Pastory Athanas, anaipatia Mbeya City bao la kwanza baada ya mabeki wa Simba SC kushindwa kumzuia.| Simba SC 3-1 Mbeya City.

City wameamka kipindi hiki cha pili huku wakipata Kona mbili ambazo haikuzaa matunda.

60' Ametoka Bwalya na ameingia Chama upande wa Simba SC huku Sangija akionyeshwa Kadi ya Njano

Athanas anaonyeshwa Kadi ya Njano baada ya kumdanganya refa eneo la 18

65' Ametoka Bocco na ameingia Kagere upande wa Simba SC. Huku City wakikosa nafasi ya kufunga.. ilikuwa hatari sana mpira wa piga nikupige.

78' Simba SC wanaongoza huku City wakijaribu kutafuta bao la pili.. Mabadiliko upande wa Simba, ameingia Mzamir nafasi ya Morrison.

85' Chama Goooooooooaaal Goooooooaaal.

Mpira mrefu uliopigwa na Nyoni unamkuta Kapombe na kutoa pasi murua kwa Clatuos Chama na kuandika bao la Nne | Simba SC 4-1 Mbeya City.

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo, huku Onyango akionyeshwa Kadi ya Njano

Nafasi ya kurudisha mabao yote kwa City yanazidi kufifia.

Naaaam umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi mnono wa mabao manne kwa moja dhidi ya Mbeya City, hivyo kuelekea kunusa harufu ya Ubingwa.

FT, VPL: Simba SC 4-1 Mbeya City.

.... Ghazwat....
 
Leo tunatarajia kuona kandanda safi ambalo ndo icon ya club ya simba.

Game iliyopita tulicheza chini ya kiwango sana licha ya kwamba tulitoka na ushindi ila ushindi haukua na stimu kwasababu zile flavour za biriani zili-miss
 
Leo tunatarajia kuona kandanda safi ambalo ndo icon ya club ya simba.

Game iliyopita tulicheza chini ya kiwango sana richa ya kwamba tulitoka na ushindi ila ushindi haukua na stimu kwasababu zile flavour za biriani zili-miss
Game ile tulichezea kwenye uwanja mbovu. Subiri uone pira biriani leo mkuu stay tuned.
 
Vikosi vya timu zote mbili ambavyo vinaumana muda mchache kuanzia sasa.
hajismanara_20210622_181705_0.jpg
Screenshot_20210622-174143.jpg
 
Bernad Morrison wa Utopolo leo ameanza.

Natamani Kakolanya aendelee kukaa golini mechi zote zilizobaki. Manula nae apumzike.
 
Leo tunatarajia kuona kandanda safi ambalo ndo icon ya club ya simba.

Game iliyopita tulicheza chini ya kiwango sana licha ya kwamba tulitoka na ushindi ila ushindi haukua na stimu kwasababu zile flavour za biriani zili-miss
Match ya leo ngumu sana
Kipa huwa hana utulivu golini, mbeya city anayataka sana matokeo is up to simba kutumia nafasi yoyoye kupata goals kipindi cha kwanza
Biriani lije dakika za mwisho kabisa
 
Bernad Morrison wa Utopolo leo ameanza.

Natamani Kakolanya aendelee kukaa golini mechi zote zilizobaki. Manula nae apumzike.
Kakolanya tatizo lake hana utulivu..
Leo anakaba Nyoni pekee
Itabidi coach aangalie dakika 30 za mwanzo hata kama ni Sub bas afanye tu
 
Back
Top Bottom