Vodacom Premier League 'VPL Uwanja wa Uhuru Dar: Simba SC 0 - 1 JKT Tanzania

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya ligi kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL kuendelea kupigwa tena leo February 7, 2020 ambapo Mnyama Mkali, Simba SC, wanawakabili JKT Tanzania.

Patashika hii ya aina yake ikiwa ni mzunguko wa pili, inatarajiwa kuwa kali na ya kusisimua kwa muda wote wa mchezo.

Simba SC kwenye mzunguko wa kwanza ameshinda mechi 16, akitoka sare 2 na kupoteza 1 huku JKT Tanzania akishinda michezo 7 sare 6 na akiwa amepoteza michezo 6.

Nani kuanza na furaha kwa duru hili la pili la VPL? Dakika 90 kuamua..Kumbuka mchezo kuanzia saa 10: 00 jioni, Usikose Ukaambiwa.

=====

Simba imepoteza mchezo wa pili msimu huu Ligi Kuu Bara baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar

Bao pekee la ushindi limefungwa na Adam Adam dakika ya 24 ya kipindi cha kwanza ambalo limedumu mpaka mwisho wa kipindi.

Nyota wapya wa Simba, Luis na Shiza Kichuya wameanza leo kwa mara ya kwanza.

Mchezo wa kwanza walipokutana Simba ilishinda mabao 3-1 na leo kisasi kimelipwa kwa JKT kushinda bao 1-0.

 
Leo nataka nimuone Luis na transformation aliyofanya kichuya baada ya kwenda kucheza soka la kulipwa nje...Marefa tu wasiharibu mechi...Simba 1 jkt 1.
 
Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Uhuru,

KICK OFF...Naaaaaaam mpira umeanza hali ya hewa tulivu kabisa, mashabiki kiasi wapo.

Simba SC Vs JKT Tanzania
 
05' JKT walifanya shambulio moja kwa shuti ambalo halikulenga lango huku Simba wakiwa wanapiga pasi za hapa na pale

Simba SC 0-0 JKT Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…