UNSPECIFIED
JF-Expert Member
- Sep 13, 2017
- 792
- 2,609
Tarehe 29/12/2022 saa tano usiku nilifanya muamala kutoka simu yangu kwenda akaunti ya benki NMB kiasi Cha 2.25m Cha kushangaza mpaka Leo hii 31/12/2022 saa saba usiku ikiwa takribani saa 27 toka nifanye muamala bado pesa haijafika NMB wala kwangu haijarudi kisingizio ni mtandao.
Nimeumizwa sana kwani hii pesa nilikuwa namlipa mteja wangu na ndio nimeshaitwa tapeli tayari.
Nimewapigia huduma kwa wateja nikatembelea Voda Shop wanasema nisubiri tena saa zingine 24 yaani hela yangu ikae pending saa 48 hivi mnaona rahisi sana?
Ninahuzunika sana na moyo wangu umepondeka kwani nimeonekana kwa mteja wangu Mimi si mwaminifu.
Hakuna namna lakini sio sawa.