Vodacom Tanzania mmeniharibia sana na M-Pesa yenu

Vodacom Tanzania mmeniharibia sana na M-Pesa yenu

Tafuta email yao watumie madai yako kwa maandishi wasipokujibu au wakikujibu na hujaridhika ndio unaenda TCRA. Ni muhimu kuweka vitu kimaandishi
Ngoja niingie kwenye website nichkue email address yao niwaandikie , Asante kwa ushauri.
 
Hii mitandao sio ya kuamini,
mimi mwenyewe nishawahi kuonekana tapeli. Kuna pesa mls 3.8 alikuwa ananidai dadangu badala ya kumlipa akassema kuna mtu amemletea mzigo so nihamishie kwenye akaunti yake.

Mimi nlikuwa nayo kwenye tigo pesa akanitumia akaunti nikahamisha na msg nikapokea ya muamala kwenda. Nikamwambia tayari naye akamtaarifu.

Ikapita siku tatu yule mtu anamwambia sista ile ela mbona haipo sista ananicheck nawapgia tigo wanasema sijui kweli haijafika kuna shida ya mtandao, kumbuka ishapita siku tatu.

Nahisi sista hakunielewa na mteja wake hakumwelewa yeye. Nimewapgia nikaona wanazingua, ikabidi niende pale ofisini kwao siku mbili wananzngua tu yan walikuja rudisha ile pesa siku ya tano toka niitume ikabidi niitoe niiweke bank lakini sister alihisi namwongopea na mteja wake alihisi anaongopewa.

Halafu wanakuwa na majibu simple kama vile wanakupa msaada
Kwa pesa serious achana na mitandao ya simu.

Wao wanaona wanakufanyia hisani.

Hasa tigopesa. Ina shida sana.

Juzi hapa nilikuwa natoa hela bank kwenda tigopesa. Hela haijafika ila kwenye account imetoka.

Baada ya siku 3 hela ikarudishwa. Sasa hapo unajiuliza kama una shida sana si ndo kwaheri?

Sahivi nikitaka kutoa hela lazima niende ATM. Hizi za simu uongo mtupu.
 
Mkuu hela ya Emergency kwa nini usiitoe na kuwapa mawakala ni rahisi tuu wala pia haina gharama hela za hivyo mimi huwa siwezi risk kwa kutoa kimtandao ni ndani au ATM mambo ya kufatilia hela yako sio poa kwa Nchi zetu ambazo mambo haya bado hizi hela za muhimu nawe zipe Umuhimu wake na Ulinzi pia...
 
Kama una shida ndio kwaheri kweli yaani kama Kuna jamaa amesema ametuma hela kwa akili ya operation ya mkewe halafu imegoma.
Inaumiza sana .
 
Mkuu hela ya Emergency kwa nini usiitoe na kuwapa mawakala ni rahisi tuu wala pia haina gharama hela za hivyo mimi huwa siwezi risk kwa kutoa kimtandao ni ndani au ATM mambo ya kufatilia hela yako sio poa kwa Nchi zetu ambazo mambo haya bado hizi hela za muhimu nawe zipe Umuhimu wake na Ulinzi pia...
Ni kweli kiongozi tunaendelea kujifunza
 
Ni kweli kiongozi tunaendelea kujifunza
Watu wanaweza kukaa na hela hata wiki mbili wanakwambia mtandao kumbe wahuni wa kitengo wanazungusha wakikaa na hela za watu 50 kwa wiki moja wanapata kiasi gani maana hao TCRA wapo busy na kusahihishq Lugha kwa vijana hizo bando tuu zinakwapuliwa na wakati bado hazijaisha na hakuna kitu kinafanyika...
 
Back
Top Bottom