Tarehe 14 January nilijiunga na kifurushi cha unlimited internet cha mwezi mzima(20000), ambacho kinatakiwa kuisha February 13.
Pamoja na kifurushi hiko, pia huwa naweka kifurushi kingine weekly Kwa ajili ya airtime ambacho pia kina mb chache za internet, ambazo huwa zikiisha naendelea kuwa na internet ile ya unlimited niliyoweka swali mpaka muda wake utakapoisha.
Jana sasa, naamka asubui nataka nifanye shughuli zangu online nashangaa internet hakuna! Huku nikijiamini kwa kuwa najua internet yangu, bado sana mpaka February nikajua labda matatizo yao YA kiufundi ambayo pia huwa hawa compensate ata SIKU moja kwa usumbufu.
Baada ya kuona hali haibadiliki nikaamua kupiga customer service, jamaa mmoja akaniambia ishu NI kwamba eti kwasababu niliweka kifurushi kingine kikaingilia kile kilichokuwepo kwahiyo kilivoisha basi kikaondoka na kile cha mwezi cha internet, na akasema habari ndo hiyo hana msaada!
Nikamueleza kuwa huwa nafanya hivo mara nyingi lakini haijawahi kutokea kifurushi changu cha internet nilicholipia 20000 kikafutika wakati muda wake bado.
Sasa nikaona hii ni too much na no wizi, Maana kuna wakati niliwahi kuweka internet ya wiki unlimited ikasepa after 2 days. Sasa nimeona huu wizi na dhuluma nikiikalia tu, watakuwa wanatuibia KILA siku, ma milioni ya watu.
Nipo kwenye early stages za kuwa sue, na kama kuna yeyote aliyedhulumiwa kwa ataivo hii ya kidigitali naomba tuwasiliane tuunde jeshi kuwakabili hawa wezi, watufidie, haiwezekani wachukue pesa bila Huduma staili.